Pambano
la kirafiki la kimataifa kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Zambia
(Chipolopolo) lililochezwa juzi (Desemba 22 mwaka huu) limeingiza sh.
109,197,000.
Fedha hizo zimepatikana kutokana
na watazamaji 17,383 waliokata tiketi kushuhudia mechi kwa kiingilio cha
sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 20,000 na sh. 30,000.
Mgawanyo wa mapato hayo ulikuwa
kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh.
16,657,169.49, maandalizi ya mchezo sh. 55,339,510, tiketi sh.
5,803,900, ulinzi na usafi kwa Uwanja wa Taifa sh. 2,350,000, Wachina
(technical support) sh. 2,000,000, umeme sh. 300,000 na maandalizi ya
uwanja (pitch marking) sh. 400,000.
Nyingine ni bonasi kwa Taifa
Stars sh. 13,826,313, asilimia 20 ya gharama za mchezo sh. 2,504,022,
asilimia 10 ya uwanja sh. 1,252,011, asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira
wa Miguu Afrika (CAF) sh. 626,005 na asilimia 65 ya Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 8,138,070.
Mapato ya mechi nyingine za Taifa
Stars ilizocheza nyumbani mwaka huu yalikuwa Taifa Stars vs Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo-DRC (Leopards) iliyofanyika Februari 23 mwaka huu
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam sh. 32,229,000. Taifa Stars vs Msumbiji
(Mambas) iliyochezwa Februari 29 mwaka huu sh. 64,714,000.
Taifa Stars vs Malawi (The
Flames) iliyochezwa Mei 26 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
iliingiza sh. 40,980,000. Taifa Stars vs Gambia (The Scorpions)
iliyochezwa Juni 10 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
zilipatikana sh. 124,038,000 na Taifa Stars vs Kenya (Harambee Stars)
iliyofanyika Novemba 14 mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza
iliingiza sh. milioni 45.
No comments:
Post a Comment