Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, December 26, 2012

RAIS KIKWETE ASHEREHEKEA KRISMASI KWA KUANGALIA MCHEZO WA SOKA KATI YA HOTELI ZA SERENA NA FOUR SEASONS MBUGANI SERENGETI


 Rais Kikwete, akisalimiana na wachezaji wakati akikagua timu hizo kabla ya kuanza kwa mchezo wa soka kati ya Four Seasons Safari Lodge na Serena, uliochezwa jana jioni wakati wa sikukuu ya Krismasi.
 Mabingwa wa Kombe la Ujirani Timu ya hoteli ya Seronera wakifurahia ushindi baada ya kuilaza kwa mabao 5-4 hoteli ya Four Seasons Safari Lodge  katika Uwanja wa Kifaru katika Hifadhi ya Serengeti mkoani Mara leo. Hadi mechi inaisha timu hizo zilitoka sare ya 1-1 kabla kupigwa mikwaju ya penati ambapo Serena walifunga mabao 4 na dhidi ya 3 ya wapinzani wao.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi nahodha wa timu ya hoteli ya Seronera Jamali Kitonga kombe la Ujirani mwema baada ya timu hiyo  kuilaza kwa mabao 5-4 hoteli ya Four Seasons katika Uwanja wa Kifaru katika Hifadhi ya Serengeti mkoani Mara leo Hasdi mechi inaisha timu hizo zilitoka sare ya 1-1 kabla kupigwa mikwaju ya penati ambapo Serena walifunga mabao 4 na dhidi ya 3 ya wapinzani wao.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...