



Mchoraji katuni, Nathan
Mpangala kwa kushirikiana wachoraji wenzake, familia, ndugu na marafiki
atatembelea watoto wanaosumbuliwa na saratani katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili, ikiwa ni muendelezo wa kazi za kijamii kufuatia Tuzo ya
Mchoraji Bora wa katuni 2011 aliyopewa na Baraza la Habari Tanzania
(MCT) na miaka sita ya Mtukwao maarufu kwa jina la Kibonzo kinachorushwa
ITV.
Ziara hiyo ina malengo yafuatayo:
Kuwapatia wagonjwa zawadi mbalimbali.
- Kuchora nao pamoja. Kwa kuwa katuni zina zinachekesha, zitawasaidia watoto hao kupunguza uwoga wa mazingira ya hospitali, zitawasahaulisha maumivu na kuwafanya kuwa bize na kufurahia siku yako.
Katika ziara hiyo Mpangala
aliambatana na baadhi ya wachoraji katuni na marafiki wa Programu ya
Wafanye Watabasamu na kuwapa zawadi watoto zawadi mbali kisha wakapata
nafasi ya kuchora nao michoro ya kawaidha na ile ihusuyo maisha yao ya
kila siku hospitalini hapo.
Kwa niaba ya watoto, Mpangala
anaishukuru familia yake, ndugu na marafiki wa Programu ya Wafanye
Watabasabu kwa zawadi mbalimbali walizochangia ambazo zimefanya ziara
hiyo kuwa ya mafanikio.
Pia anashukuru wachoraji wote
waliojitokeza na kuungana naye Muhimbili kwani uwepo wao ulirahisisha
usimamiaji wa zoezi la uchorajikwani kila mtoto alisikilizwa pale
alipohitaji maelekezo hivyo kufanya watoto.
No comments:
Post a Comment