BAADA ya Waziri wa Ofisi ya
Makamu wa Rais (Mazingira), kuwashukia viongozi wa jiji kuwa ndiyo
chanzo cha kukithiri uchafu jijini, Meya wa jij
Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar
es Salaam mwishoni mwa wiki, na Meya huyo wakati alipokuwa akizungumza
na wandishi wa habari kuhusu kikao cha kufunga mwaka 2012.
Masaburi alisema kauli ya waziri
huyo, inaonekana kujichanganya kwani kazi ya kuliweka jiji hilo katika
hali ya usafi siyo ya jiji bali wahusika wakuu ni Halmashauri.
Alisema kazi kubwa ya mamlaka ya jiji ni kusimamamia hali ya usafi usafi wa dampo liliko Pugu Kinyamwezi.
“Hizo lawama wanapaswa
wazielekeze kwenye Halmashauri kutokana na wenyewe kushindwa kupeleka
taka na siyo sisi jiji, kama wenyewe hawatuletei taka dampo na
alaumiwe”alisema.
Dk Masaburi anastajabishwa,
utaratibu unaotumiwa na baadhi ya mawaziri kwa kuzishambulia Halmashauri
kuwa zinafuga uozo wa uchafuzi wa mazingira, ambapo hata huko kwenye
ofisi za wizara zao upo uchafu.
Alitoa wito kwa Serikalli Kuu
kubadili utaratibu wake kwa kuzitengea fedha za kutosha Halmashauri hizo
na kuzifikisha kwa wakati, lengo likiwa ni kwenda sambamba na sheria
ya mazingira ya mwaka 2004.
Alisema vyanzo ya mapato wakati
mwingine vinaweza kuwa chanzo cha Halmashuri hizo kushindwa kusimamia
sheria hiyo ya utunzaji wa mazingira.
No comments:
Post a Comment