Mshambuliaji wa Simba Uhuru Seleman akiwani mpira dhidi ya kiungo wa
Tusker ya Kenya Joseph Mbugi wakati wa mchezo wa kirafiki uliopigwa
uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam na Simba kukubali kutandikwa bao
3-0.
SIMBA SC imefungwa mabao 3-0 na Tusker ya Kenya katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika
mchezo huo, uliochezeshwa vema na refa Hashim Abdallah, hadi mapumziko,
tayari Tusker walikuwa mbele kwa mabao 2-0, yaliyotiwa kimiani na Jesse
Were dakika ya 37 na 45.
Mabao
yote yalitokana na udhaifu wa safu ya ulinzi ya Simba, ambayo hii leo
iliongozwa na beki kutoka Mali, Komabil Keita kiasi cha kufikia mfungaji
anafunga akiwa amebaki anatazamana na kipa.
Simba
ilikuwa ikishambulia kutokea pembeni, lakini mipira mingi mirefu
iliyokuwa inamiminwa langoni mwa Tusker ilikuwa inaokolewa na mabeki
warefu wa klabu hiyo bingwa ya Kenya, wakiongozwa na beki wa zamani wa
Yanga, Joseph Shikokoti.
Kipindi cha pili, Tusker walirudi kwa nguvu tena na kufanikiwa kupata bao la tatu dakika ya 54, mfungaji Frederick Onyango.
Simba
pamoja na kufanya mabadiliko, ikiwatoa Haruna Shamte, Haruna Athumani,
Paul Ngalema, Mussa Mudde, Abdallah Seseme, Abdallah Juma, Ramadhani
Chombo na Kiggi Makassy na kuwaingiza Miraj Adam, Hassan Isihaka, Emily
Ngeta, Jonas Mkude, Salim Kinje, Haruna Moshi, Ramadhani Singano, Nassor
Masoud ‘Chollo’ na Edward Christopher, haikuweza kupata hata bao la
kufutia machozi.
Nassor
Masoud aliingia kuchukua nafasi ya Shamte, lakini naye akaumia na
kutoka nafasi yake ikichukuliwa na kinda wa Simba, B, Masele Kaheza.
Simba SC; William
Mweta, Haruna Shamte, Paul Ngalema, Hassan Khatibu, Komabil Keita,
Mussa Mude, Haroun Athumani, Abdallah Seseme, Abdallah Juma, Ramadhan
Chombo na Kiggi Makassy.
Tusker FC; Samuel
Odhiambo, Luke Ochieng, Jeremiah Bright, Mark Odhiambo, Joseph
Shikokoti, Khalid Aucho, Edwin Manono, Frederick Onyango, Ismail Dunga,
Jesse Were, Robert Omonuk,
No comments:
Post a Comment