|
Mgeni rasmi Edson Fungo akikata utepe kuashiria uzinduzi wa tawi la Napoli |
|
Wageni wakitazama wanachama wakicheza pamoja na matarumbeta (hawapo kwenye picha) |
|
Baadhi ya wachezaji wa Ashanti wakiwa wapo pamoja na wanachama wa Ashanti |
|
Ashanti haichagui rangi kwani haina wenyewe, wenyewe ni wale wote wenye mapenzi mema nayo |
|
Almas Kasongo ambaye ni Mwenyekiti wa DRFA akiongea kwenye hafla hiyo |
|
Khalfan Suleiman akitoa maoni yake |
|
Rais wa tawi la Napoli Ally Mahmoud akiwa amebebwa na wanachama wa tawi hilo |
|
Wanachama wa Napoli |
|
Ally Mahmoud, Rais wa tawi la Napoli akiongea |
|
Mwanachama akipokea kadi yake |
|
Mwenye kiti wa serikali za mitaa akipokea kadi yake |
|
Wachezaji na baadhi ya mashabiki wakiwa na kocha Mubaraka Hassan |
|
Wachezaji na benchi la Ufundi |
|
Mgeni rasmi akiwapongeza wachezaji kwa kuwashika mikono |
|
Almas Kasongo |
|
Mgeni rasmi Diwani wa Ilala, Edson Fungo akiongea na wanachama na mashabiki wa Ashanti |
|
Mgeni rasmi akipata maakuli pamoja na wenyeji wake |
|
Biriani tamu hadi wanalisikilizia |
|
Wachezaji nao hawakuwa nyuma, cheki plate zilivyojaa halafu mmoja kakamatia peke yake |
WANACHAMA wa timu ya Ashanti United inayoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara,
msimu ujao wamezindua tawi la kwanza kuanzia timu hiyo ianzishwe kwa ajili ya
kutoa hamasa na kuiwezesha kiuchumi timu hiyo jana.
Tawi hilo linaitwa Napoli na lina wanachama 55 limezinduliwa
kwenye mtaa wa Kilwa na Utete, Ilala na Diwani wa Kata ya Ilala kupitia Chama
Cha Mapinduzi (CCM). Edson Fungo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyohudhuriwa na wachezaji
wa Ashanti, wanachama na viongozi wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam,
Edson Fungo ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi, aliwataka wanachama hao kufuata
katiba ya timu na siyo kuendesha tawi kwa manufaa yao bali ya klabu.
“Nimefurahi kuona mmeguswa na kuanzisha tawi hili hivyo na
mimi nitakuwa mwanachama, lakini msiache majukumu yenu kama wanachama badala ya
kusaidia Ashanti mkajisaidia wenyewe na kuleta migogoro”, alisema Fungo.
Pia aliwataka wachezaji wacheze kwa kujituma wakijua kuwa
mpira ndio ajira yao ambayo itawasaidia katika maisha yao ya baadae.
Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam, Almas Kasongo
alisema amefurahishwa na wanachama hao kuona wanawiwa kuona Ashanti
inafanya vizuri na kuwaahidi atakuwa pamoja nao ili Ashanti isiwe
inakwenda kucheza ligi kuu na baadae kurudi tena daraja la kwanza.
Naye Rais wa tawi hilo la Napoli, Ally Mahmoud alisema kuwa
tawi lao litakuwa na kazi ya kuisaidia timu kiuchumi kwani wanachama watakuwa
wanalipa ada ambazo zitakuwa zinakwenda kusaidia timu.
“Mpira unaendesha kwa kutumia pesa hivyo sisi kama mashabiki
wa Ashanti tumeguswa tukaona namna ya kuisaidia timu ni kuanzisha tawi hili ili
kila mwanachama achangie timu”, alisema Mahmoud.
Wanachama wa tawi hilo walikabidhiwa kadi zao kisasa na mgeni rasmi na kuahidi kuwa wanachama
watiifu kwa uongozi na timu yao.
No comments:
Post a Comment