Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani Tanzania,Mohamed Mpinga akiongea na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Mapambano , kuhusiana na masuala ya Usalama Barabarani katika kuadhimisha wiki ya Umoja wa Mataifa ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo
huadhimishwa Mei 6 hadi 12 ,ambapo wafanyakazi wa vodacom waliambatana
na mkuu huyo katika kutoa elimu kwa watoto wa shule hiyo na Uzuri zote
za Sinza jijini Dares Salaam na kutoa msaada wa madafutari na vitabu
mbalimbali vya kujisomea,anaeshuhudia kulia ni Meneja uhusiano wa nje wa
Vodacom Tanzania,Bw.Salum Mwalim.
Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania,Bi.Ena Mwangama,akimkabidhi kitabu cha sayansi mmoja wa wanafunzi wa shule ya Mapambano iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam, wakati wafanyakazi wa vodacom Tanzania,walipofika shuleni hapo kutoa elimu ya Usalama
Barabarani ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa
ya Nenda kwa Usalama Barabarani yaliyoanza Mei 6 hadi 12.kila mwaka.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania , wakiwafundisha wanafunzi wa shule
ya msingi ya Mapambano ya jijini Dar es Salaam, baada ya kuwapa msaada
wa vitambu vya sayansi ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Umoja
wa Mataifa ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo huadhimishwa Mei 6
hadi 12 ,ambapo wafanyakazi wa vodacom waliambatana na mkuu wa kikosi
cha Usalama barabarani Tanzania,Mohamed Mpinga (hayupo pichanini) kutoa
elimu kwa watoto wa shule za Uzuri na Mapambano zote za Sinza jijini
Dares Salaam.
Meneja
wa Vodacom Tanzania Grece Lyon (kushoto ) na Mwalimu Mkuu wa shule ya
msingi Uzuri Tandale ya jijini Dar es Salaam, (kulia)wakionyeshwa vitabu
vya sayansi na wanafunzi wa shule hiyo baada ya kukabidhiwa na
wafanyakazi wa Vodacom, Ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya wiki ya Umoja
wa Mataifa ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo huadhimishwa Mei 6
hadi 12 ,ambapo wafanyakazi wa vodacom waliambatana na mkuu wa kikosi
cha Usalama barabarani Tanzania,Mohamed Mpinga (hayupo pichanini) kutoa
elimu kwa watoto wa shule za Uzuri na Mapambano zote za Sinza jijini
Dares Salaam.
Meneja
Mawasiliano wa Vodacom Rukia Mtingwa akiwaongoza wanafunzi wa shule ya
msingi ya Uzuri iliyopo Tandale jijini Dar es Salaam, kwenda kujifunza
jinsi ya kutumia alama za barabarani ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya
Umoja wa Mataifa ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo huadhimishwa Mei
6 hadi 12 ,kila mwaka .Wafanyakazi wa Vodacom waliambatana na Mkuu wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Tanzania,Mohamed Mpinga (hayupo pichanini) Pia walitoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo vitabu vya Sayansi.
No comments:
Post a Comment