Meneja
Matukio wa Dar Live, Abdallah Mrisho (wa pili kushoto) akiongea na
wanahabari (hawapo pichani) wakati wa utambulisho huo. Wengine pichani
kutoka kushoto ni DJ John Dilinga (JD), Prodyuza Ally Baucha na Prodyuza
Tudd Thomas.
Kutoka kushoto waliokaa ni msanii Stamina, DJ John Dilinga, Abdallah
Mrisho, Ally Baucha na Tudd Thomas katika picha ya pamoja na washiriki
wa The Vodacom Mic King waliosimama nyuma.
Uongozi
wa Dar Live Co. Ltd leo umetambulisha tamasha kubwa la kila mwaka la
Usiku wa Hip Hop na fainali za kumtafuta Mkali wa Mic zijulikano kama
'The Vodacom Mic King' kwa wanahabari.
Tamasha
hili litafanyika Jumamosi hii, Mei 25, 2013 katika Uwanja wa Taifa wa
Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar. Jumla ya vijana
tisa wenye vipaji watapanda stejini kuchuana na mshindi ataondoka na
gari aina ya Toyota Funcargo (New Model) yenye thamani ya shilingi
milioni 15.
Mbali
na zawadi ya gari, mshindi wa kwanza, pili na watatu, watapata fursa ya
kurekodi wimbo mmoja chini ya Prodyuza mahiri nchini, Tudd Thomas,
aliyerekodi wimbo maarufu wa Leka Dutigite wa Kigoma All Stars na
nyingine nyingi. Majaji katika shindano hili ni mwandishi mkongwe wa
habari za muziki na wasanii, Abdallah Mrisho, DJ John Dilinga (JD) na
Prodyuza Ally Baucha.
Tamasha
hilo litapambwa na burudani kutoka kwa wakali wa Hip Hop nchini ambao
ni Fid Q, Joh Makini, Stamina, Kala Jeremiah, Nay wa Mitego pamoja na
shoo kali kutoka kundi la Wakali Dancers. Katika usiku huo, zitatolewa
tuzo kwa wasanii wa Hip Hop na kwa wimbo bora wa Hip Hop uliofanya
vizuri mwaka 2012/13. Kutakuwa na Tuzo kwa Msanii Mkongwe Bora wa Hip
Hop na Msanii Chipukizi Bora wa Hip Hop pamoja na Wimbo Bora wa Hip Hop.
No comments:
Post a Comment