Meneja
Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Fimbo Butallah akizungumza na
Waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati akitangaza zawadi kwa
Mshindi wa Kwanza wa Ligi Kuu ya Grand Malt Zanzibar 2013/14,katika
ukumbi wa Mikutano wa Kilimanjaro House,Masaki jijini Dar es Salaam
leo.Kushoto ni Meneja wa Kinywaji cha Grand Malt ambao ndio wadhamini
wakuu wa Ligi kuu ya Zanzibar,Consolata Adam.
Na Mwandishi Wetu
WADHAMINI
wakuu wa Ligi Kuu ya Zanzibar, kinywaji cha Grand Malt jana walianika
rasmi kombe atakalokabidhiwa mshindi hapo kesho, huku kukiwa na
maandalizi ya sherehe za ‘kufa mtu’.
Mshindi
anayetarajiwa kukabidhiwa kombe hilo ni KMKM ambayo ndiyo imefanikiwa
kulitwaa taji hilo msimu huu, huku ikitarajiwa pia kuondoka na kitita
cha Sh milioni 10.
Katika
hafla fupi ya kulionesha kombe hilo iliyofanyika katika ofisi za Grand
Malt, Dar es Salaam, Meneja Masoko wa kinywaji hicho, Fimbo Butallah
alisema kwao ni heshima kubwa kudhamini Ligi Kuu ya Zanzibar, ambayo kwa
sasa ina ushindani mkubwa.
“Sherehe
ya kumkabidhi mshindi taji itafanyika keshokutwa (kesho) katika Uwanja
wa Amaan, ambapo kutakuwa na pambano la kufunga ligi kati ya KMKM na
Zimamoto,” alisema Butallah.
Kwa
mujibu wa Butallahatakabidhiwa taji hilo na Makamu wa Pili wa Rais,
Balozi Seif Ally Idd, ambapo kutakuwa na shamrashamra za kila aina.
Mbali
na kupata kombe na fedha, mshindi atapata pia medali, huku mshindi wa
pili akiondoka na Sh milioni 5 na medali ambazo zitatolewa na wadhamini
wa ligi hiyo, Grand Malt.
Akizungumzia
kuhusu maandalizi ya kufunga ligi hiyo, Meneja wa Grand Malt, Consolata
Adam alisema, kila kitu kimekamilika na wamejipanga kuwapa burudani ya
aina yake wakazi wa Zanzibar.
“Tumeandaa
vikundi mbalimbali vitakavyotoa burudani uwanjani tangu saa 7 mchana,
ikiwemo vikundi vya sarakasi na ngoma maarufu ya Kidumbati hivyo
tunawaomba watu wafike mapema uwanjani ili kuweza kupata burudani hizi.”
Grand
Malt wameamua kufanya kjufuru zaidi kwani mchezo huo hautakuwa na
kiingilio, ili kutoa fursa kwa wapenzi wote wa soka Zanzibar washuhudie
jinsi bingwa mpya anavyokabidhiwa kombe.
Grand
Malt ndiyo wadhamini wakuu wa ligi hiyo inayojulikana kama ‘Grand Malt
Premier League’ na wameidhamini kwa muda wa miaka mitatu.
No comments:
Post a Comment