Rais Jakaya Kikwete (kushoto) akiteta jambo na mbunge wa jimbo la Isimani Wiliam Lukuvi leo
watumishi wa mahakama kuu kanda ya Iringa pia wamepata kushiriki
..............................................................................
MBUNGE wa jimbo la Isimani wilayani Iringa mkoani Iringa Bw. Wiliam
Lukuvi amempongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kuwawezesha wakazi wa tarafa
ya Isimani kuweza kuanza kushuhudia mapinduzi makubwa ya kimaendeleo kupitia
mradi mkubwa wa barabara ya kiwango cha lami kutoka Iringa - Dodoma
inayopita katika tarafa hiyo .
Lukuvi ambae ni waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu (sera na
uratibu wa bunge) alisema kuwa barabara hiyo ambayo ni ukombozi mkubwa kwa
nchi za kusini mwa Tanzania ilikuwemo katika mkakati wa kujengwa kwa
kiwango cha lami kwa kitambo kirefu na kila awamu wananchi walikuwa
wakiulizana juu ya kuanza kwa mradi huo.
Hata hivyo alisema baada ya awamu hii ya nne chini ya Rais Kikwete
wananchi hao wameweza kushuhudia majibu ya maswali yao kwa kuanza kwa
ujenzi huo ambao kila mmoja anatambua kama ni ukombozi katika sekta ya
maendeleo.
Waziri Lukuvi alitoa pongezi hizo kwa Rais Kikwete leo wakati
akiwasalimia wananchi wa jimbo la Isimani ambao walishiriki hafla fupi ya
Rais Kikwete kuweka jiwe
Kwa upande wake Rais Jakaya Kikwete
alisema kuwa mbali ya serikali kujipanga kwa ujenzi wa barabara
bado lengo la serikali ni kuhakikisha nchi nzima inaunganishwa kwa
mtandao wa barabara ya lami na kuwa kazi hiyo tayari imeanza.
Alisema kuwa serikali yake toka
imeingia madarakani imeendelea kuongeza fedha katika mfuko wa
barabara na kuwa lengo ni kuendelea kuongeza zaidi fedha katika
mfuko huo ili kuwezesha ujenzi wa barabara nchini kuweza
kukamilika
Rais Kikwete pia amewapongeza
viongozi wa TANROADS kwa kazi nzuri wanayoendelea kuifanya na kwa
mbali ya kupongezwa bado hawapaswi kulewa sifa na badala yake
kuendeleza jitihada za kusimamia kazi hiyo kwani upo usemi unao sema
kuwa mgema akisifiwa pombe huweka maji .
Pia Rais Kikwete alimpompongeza waziri
wa fedha Dkt Wiliam Mgimwa kwa kuendelea kuidhinisha fedha kwa ajili
ya miradi ya barabara hapa nchini na kuwa bila wizara hiyo kutenga
bajeti kazi hiyo ingeendelea kuwa ngumu.
|
No comments:
Post a Comment