Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.
Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Ndugu. Adam H. Mayingu tuzo ya kuwa Mfuko wa kwanza wa Hifadhi ya
Jamii Tanzania kutoa mikopo ya nyumba kwa wanachama wake. Tuzo hiyo ilitolewa kwenye maadhimisho ya
kilele cha Wiki ya Mifuko ya Jamii mjini Dodoma. Mh. Raisi alisema PSPF ni mfuko madhubuti na
una fursa nyingi za kimaendeleo kwa wananchi wa Tanzaniai na unauwezo mkubwa na
salama katika uwekezaji . Aliongezea kwa
kusema sio kweli kwamba Mfuko huu uko mahututi kama ilivyozungumziwa kwenye
baadhi ya vyombo vya habari, bali Mfuko huu unadai wadai wake Trilioni 6 na
kudai sio kufilisika tena
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete akisoma kipeperushi cha nyumba za PSPF
zinazokopeshwa kwa wanachama wa Mfuko huo, huku akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko huo ndugu Adam H. Mayingu
akimuelezea kuhusu nyumba hizo na fursa zingine zilizopo PSPF kwa Watanzania
ikiwa ni pamoja na ujumbe kwa Watanzania kwamba mtu yeyote mwenye umri
usiopungua miaka 18 anaweza kuwa mwanachama wa PSPF
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa
Pensheni wa PSPF ndugu Adam H. Mayingu akimuelezea Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr.
Rehema J. Nchimbi kuhusu shughuli za Mfuko na fursa zilizopo kwa watanzania
hususani mikopo ya nyumba na mafao ya aina mbalimbali ikiwemo fao la
Ujasiliamali na Elimu.
Mtangazaji wa TBC Amina Mollel
akikabidhi fomu ya kujiunga na PSPF kwa Meneja Masoko wa Mfuko huo Bi.
Costantina Martin mala baada ya kuvutiwa na kukata shauri ya kuwa mwanachama wa
Mfuko wa kwa njia ya uchangiaji wa hiari
Timu ya PSPF iliyokuwa kwenye
maonyesho ya wiki ya hifadhi ya Jamii wakiwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wao ndugu
Adamu Mayingu katikati. Timu hiyo
inastahili pongezi kutokana na uduma bora waliyokuwa wakiitoa kwa wananchi
waliokuwa wakitembelea banda hilo la PSPF pale Nyerere squire Dodoma.
Wanachama
wa PSPF wakipata taarifa mbalimbali ikiwapo historia ya michango yao na taarifa
za uanachama.
No comments:
Post a Comment