Na
Elizabeth John
KOCHA wa
timu ya taifa ya ngumi, Remmy Ngabo, ameitaka serikali na wadau wa ngumi nchini,
kujitolea kudhamini kambi ya mabondia 16 ambao
wanajiandaa na mashindano ya Majiji yanayotarajia kufanyika Julai 1 hadi 7
mwaka huu, jijini Mwanza.
Awali mashindano hayo yalipangwa kufanyika Juni 20 hadi 25,
kutokana na kutokuwa na maandalizi ya kutosha, wamelazimika kusogeza mbele
tarehe ya kufanyika kwa mashindano hayo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, alisema mabondia hao
kwasasa wanaendelea na mazoezi ya kujifua katika uwanja wa Taifa wa Ndani
jijini Dar es Salaam kwaajili ya maandalizi ya michuano hiyo.
“Mabondia wapo katika hali ngumu ya maandalizi hivyo wadau wa
mchezo huu tunawaomba wajitokeza kudhamini maandalizi haya,” alisema.
Alisema mashindano hayo ya Majiji ni maandaliazi ya kuwaweka sawa
mabondia kwaajili ya mashindano ya Afrika na Olimpiki ambayo yanatarajia
kufanyika hivi karibuni yakishirikisha mataifa mbalimbali.
No comments:
Post a Comment