Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, May 16, 2013

JAJI MKUU WA TANZANIA AELEZA MIKAKATI YA KUBORESHA MAHAKAMA KUU NCHINI .....


Jaji  mku wa Tanzania Mhe.Mohamed Chande
............................................... 
Na Elizabeth Ntambala
Sumbawanga
JAJI mkuu wa Tanzania Mohamed Chande  amesema kuwa mahakama  kuu Tanzania inaendelea na mkakati endelevu wa miaka 2 utakao husisha unoreshajki wa miundombinu ya mahakama za ngazi zote nchini kutoa elimu ya kujiendeleza kwa watumishi wake na pia kuzitolea uamuzi kesi zote zilizochukua mda mrefu.

Jaji mkuu  Mohamed Chande  aliyasema hayo alipokuwa katika ziara yake ya kikazi ya siku ya kwanza ya kukagua maendeleo ya utendaji haki kwa mahakam ya mikoa ya Rukwa na Katavi.

Jaji mkuu wa Tanzania Mh. Mohamed alisema kuwa utekelezaji wa mkakati huo ni moja ya miundombinu za kuondoa usumbufu wanaoupata wananchi wakati wa uendeshaji wa kesi zao na pia kuondoa lawama za muda mrefu za uwajibikaji mdogo na vitendo vya rushwa.

Akiongea na watumishi wa mahakama hizo za hakimu mkazi wilaya na mkoa na baadae watumishi wa mahakama kuu kanda ya sumbawanga alidai kuwa zaidi ya shilingi bilioni 10 zinategemewa ku[itishwa katika mwaka huu wa fedha wa utekelezaji mkakati.

Kwa upande wake hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Manase Goroba alisema kumekuwepo na changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo hasa ya wapiga chapa ikiwamo ya uchakavu wa majengo mengi ambayo yanahitaji ukarabati mkubwa katika mahakama .

Alisema kuwa kumekuwepo na mahakama mpya ambazo ni zilijengwa kwa nguvu za wananchi na bado majengo hayo hajakamilika hivyo kunahitaji fedha kwa ajili ya umaliziaji wa majengo hayo.
Mustafa sijani ni hakimu wa mwanzo wa wilaya walimweleza jaji mkuu kuwa adha zinazowakabili watumishi wa mahakama katika utendaji wa kazi ni pamoja na uhaba wa watumishi vitendea kazi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...