Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amosi
Makalla (mwenye suti) akifurahi pamoja na wachezaji wa chuo cha St.John’s mara baada ya kutwaa ubingwa wa ‘Safari Lager
Higher Learing Pool Competition 2013’
Mkoa wa Dododma.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amosi
Makalla (katikati) akimkabidhi nahodha wa chuo kikuu cha St.John’s, Mkole
Mpangala fedha taslim Sh.500,000 mara
baada ya kutwaa ubingwa wa mashindano ya ‘Safari Lager Higher Learing Pool
Competition 2013’ katika mkoa wa Dodoma,
(wa pili kushoto), mwenyekiti wa chama cha mchezo huo mkoani hapa (DOPA),Fred
Mushi.
CHUO kikuu cha
St.John's, juzi kilifanikiwa kutetea ubingwa wake wa mashidano ya mchezo wa
pool kwa wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani hapa ya 'Safari Lager Higher Learning
Pool Competition 2013' baada ya kukifunga chuo kikuu cha UDOM magoli 13-3
katika mchezo wa fainali ya mashindano hayo.
Mashindano
hayo ambayo mgeni rasmi alikuwa ni Naibu
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amosi Makalla, yalifanyikia
kwenye wa Royal Village.
Jumla ya vyuo vikuu
vinne vya mkoani hapa vilishiriki mashindano hayo ambayo yanadhaminiwa na
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager.
Chuo cha St. John's
kwa kutwaa ubingwa huo kwa mwaka wa pili mfululizo licha ya kujinyakuia fedha
taslim Sh.500,000 pia kitauwakilisha mkoa wa Dodoma katika fainali za taifa
ambazo zitafanyika kuanzia Juni mosi mwaka huu jijini Dar es salaam.
Fainali hizo
zitashirikisha vyuo vinane ambavyo vitaibuka mabingwa kwenye mikoa yao ngazi ya
mikoa ya mashindano hayo.
Chuo cha UDOM kwa
kushika nafasi ya pili kilizawadiwa Sh.300,000 huku chuo cha CBE kilichoshika
nafasi ya tatu kiliondoka na Sh.200,000 na chuo cha Mipango kilipewa Sh.100,000
baada ya kushika nafasi ya nne.
Kwa upande wa
mchezaji mmoja mmoja (wanaume), Juma Daniel wa chuo cha Mipango alitwaa ubingwa
huo na kujinyakulia fedha taslim Sh.150,000 na tiketi ya kushiriki fainali za
taifa na Abdallah Abdallah wa chuo cha UDOM
aliyeonyesha kiwango cha hali ya juu na kujifunga kwa bahati mbaya
alishika nafasi ya pilli na kupewa Sh.100,000.
Remi Jackson wa
chuo cha UDOM naye alifanikiwa kutetea ubingwa wake kwa mchezaji mmoja
(wanawake) na hivyo kujinyakulia Sh.100,000 na tiketi ya kushiriki fainali za taifa za mashindano hayo na Mwanaisha
Abdallah wa chuo cha CBE alipewa Sh.50,000 kwa kushika nafasi ya pili.
Kabla ya kukabidhi
zawadi kwa washindi, Naibu Waziri wa Habari,VIjana, Utamaduni na Michezo, Amosi
Makalla aliwapongeza wadhamini wakuu wa
mchezo huo nchini, bia ya Safari Lager kwa kuweza kuuinua mchezo huo na kuufikisha
hapa ulipofika.
Makalla pia
aliwapongeza viongozi wa vyama vya mchezo huo kuanzia wilaya hadi taifa kwa
ushirikiano wao ambao umeendelea
kumvutia mdhamini kuendelea kuudhamini mchezo huo bila ya kurudi nyuma..
"Ni vema
mkaendeleza amani na ushirikiano mlionao sasa ili mchezo wa pool uendelee
kumvutia kila Mtanzania, kwa kweli ni mchezo mzuri ambao na mimi nitaanza
kujifunza.
Nakwa upande wa
serikali inautambua kama ilivyo michezo mingine na wizara itaendelea kuwaunga
mkono katika kuuendeleza zaidi ili siku moja uweze kuiletea heshima Tanzania
katika mashindano ya kimataifa,"alisema Makalla.
No comments:
Post a Comment