Wasanii wa muziki wa kizazi kipya Diamond na Ney wa Mitego wakitumbuiza jukwaani kwenye uzinduzi wa tamasha la Epiq Open Mic
======= ====== ========
Katika kuelekea msimu wa sita wa
shindano la kuimba la Epiq Bongo Star Search, kampuni ya simu za
mikononi ya Zantel leo imezindua Epiq Open Mic ikiwa ni nafasi nyingine
kwa vijana wenye vipaji vya muziki kuonyesha vipaji vyao kabla usaili
wa Epiq Bongo Star Serach haujaanza.
Epiq Open Mic inatarajiwa
kuwapa nafasi vijana kujifunza misingi ya muziki kutoka kwa mmoja
wa watayarishaji wa muziki maarufu zaidi nchini, Marco Chali. Marco
Chali ambaye pia ni mtunzi na mwimbaji, ametayarisha nyimbo
nyngi ambazo zimeshinda tuzo ndani na nje ya nchi za wasanii kama Ms.
Trinity kutokea Jamaica, A.Y
wa Tanzania, Prezzo wa Kenya, J Martins kutoka Nigeria na
wengine wengi. Tamasha hilo la Epiq Open Mic, ambalo ni la bure
litazinduliwa rasmi kwenye viwanja vya Mwembe Yanga Temeke
tarehe 26 ya mwezi huu ikisindikizwa na wakali kibao wa Bongo
flavor kama Diamond Platnumz, Madee, Godzila, Ney wa Mitego,
Mabeste na Mrap.
Akizungumza wakati wa kuzindua
matamasha hayo, Afsa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan alisema
kampuni ya Zantel inaaminini katika kuwawezesha vijana kufikia ndoto
zao. ‘Muziki ni ajira kwa vijana wengi, na kuamini hilo ndio maana
kampuni ya Zantel imeamua kuwafikia vijana wote wenye vipaji na
kuwapa nafasi ya kuonekana’ alisema Khan.
Baada ya uzinduzi wa tamasha
la Epiq Open Mic Mwembe Yanga tamasha hilo litaendelea kila
jumamosi kwenye makao makuu ya Zantel likiwapa nafasi vijana
kujisajili na kurekod sauti zao. Vijana watakaorekodi sauti zao
watapigiwa simu na timu ya watayarishaji wa muziki chini ya Marco Chali
pamoja na wanamuziki ili kuwapa ushauri wa namna ya kuboresha muziki
wao zaidi.
‘Zantel imejipanga kutumia fursa
hii kuwahamasisha vijana kushiriki katika kukuza vipaji vyao,
kuongeza uelewa wa mambo ya muziki pamoja na kuchangamkia fursa
zilizopo katika muziki’ alisisitiza Khan. Epiq Open Mic pia
inatarajia kuwapa fursa ya kurekodi baadhi ya vijana watakaokua
na vipaji.
No comments:
Post a Comment