Press Release
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es
Salaam, Ramadhani Madabida atakuwa mgeni rasmi katika tamasha la Mastaa
chipukizi zaidi ya 320 litafanyika Jumapili 26, 2013 katika ukumbi wa Starlight
Hotel kuanzia saa 4 asubuhi.
Peter Mwenda |
Mwenyekiti wa Shiwata, Caasim Taalib alisema Madabida
ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) atapata nafasi ya kuona vikundi
mbalimbali vya sanaa kikiwepo kikundi cha Kaole, Splendid, Super Shine Taarab pamoja na
wasanii mbalimbali wa Bongo Flava, Maigizo,Ngoma, Dansi na Sarakasi nao wamethibitisha
kushiriki.
Taalib alisema wasanii wakongwe wa bongo flava walioalikwa
ni Stara Thomas, Safi Theatre Group, Ommy G na waigizaji wakongwe wa Kaole na
Splendid wataonesha umahiri wao katika fani ya sanaa Kauli Mbiu ikiwa ni Kilio
cha Msanii .
Vikundi vingine vitakavyonesha vipaji vyao ni Kepteni Shaibu, Tanzania Disabled, Uyoga Boga
Village, Ndafu Arts Group, CGC, Magengistar Crew, Dodo Arts Group, Culture Arts
Group, Wachapa Kazi Academy, Soweto Picture, Shiwata Commedy, Mwavionelachi, Manuari
Arts Group, Tandale Morden Taarab na Begeja Wushu,
Taalib alisema tamasha hilo ambalo limepata
kibali cha Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) pia wamealikwa Shirikisho la Sanaa
za Maonesho Tanzania,Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF),Shirikisho la Muziki
Tanzania na Shirikisho la Sanaa za maonesho Tanzania.
Mwenyekiti aliwaomba viongozi wengine wa bendi za
muziki, taarab, vikundi vya sanaa,mapromota,maprodusa na wadau wote kushiriki
katika tamasha hilo
ili kujenga ushirikiano wa pamoja.
Peter Mwenda
Ofisa Habari wa SHIWATA
0715/0752-222677
No comments:
Post a Comment