Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi (kushoto) akisalimiana
na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Hamis
Mdoe alipowasili kuindua Bodi mpya ya Wakurugenzi wa NHIF, leo kwenye
Hoteli ya Courty Yard, Sea View, Dar es Salaam. Wengine ni Mwenyekiti
mpya wabodi hiyo, Balozi Ali Mchumo (wa pili kushoto), Mkurugenzi Mkuu
wa NHIF, Emmanuel Humba na Kaimu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Regina
Kikoli.
Wakurugenzi wa NHIF, wakipiga makofi wakati Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Mwinyi alipokuwa akiingia kuzindua bodi hiyo.
Dk. Mwinyi akihutubia wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo.Kulia ni Mwenyekiti wa bodi hiyo, Balozi Mchumo.
Baadhi ya mameneja wa Mikoa wa NHIF, na maofisa wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa bodi hiyo.
Mwenyekiti
mpya wa Bodi hiyo, Balozi Mchumo (kushoto) akimshukuru Waziri, Dk.
Mwinyi kwa kuzindua bodi hiyo.Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo,
Humba.
Mkurugenzi
Mkuu wa NHIF, Emmanuel Humba akitoa maelezo kuhusu utendaji wa mfuko
huo, Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,
Regina Kikoli
Mwenyekiti mpya wa Bodi ya NHIF, Balozi Ali Mchumo akuhutubia wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo.
Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi (wa nne kushoto
waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi mpya ya NHIF.
Kutoka kushoto ni Mwanaidi Mtanda,Donnan Mmbando, Mwenyekiti Balozi Ali
Mchumo, Mohammed Hashim, Charles Kajege, Dk. Ali Mohammed na Naibu
Katibu Mkuu wa wa wizara hiyo, Regina Kikoli.Waliosimama ni Mkurugenzi
Mkuu, Emmanuel Humba (kulia na Naibu Mkurugenzi Mkuu, Hamis Mdoe.
Waziri Dk. Hussein Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi pamoja na wakurugenzi wa NHIF.
Waziri, Dk. Hussein Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya mameneja wa NHIF wa mikoa.
Waziri, Dk. Hussein Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Mameneja wa NHIF wa mikoa.
Dk.Mwinyi
akibadilishana mawazo na Mwenyekiti mpya wa bodi hiyo, Balozi Ali
Mchumo (kushoto) pamoja na Mjumbe wa bodi hiyo, Mohammed Hashim.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Regina Kikoli (kulia)
akiagana na Balozi Ali Mchumo. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NHIF,
Emmanuel Humba. Picha zote na Kamanda wa Matukio)
Na Grace Michael
WAZIRI
wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi amesema ni wakati
muafaka sasa kwa kuwa na chombo kimoja kitakachokabidhiwa jukumu la
kusimamia bima ya afya kwa Watanzania badala ya kushughulikiwa na
taasisi nyingi kama ilivyo hivi sasa.
Dk.
Mwinyi ameyasema hayo Dar es Salaam leo wakati akizindua bodi mpya ya
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ambapo ameitaka bodi hiyo
kuangalia uwezekano wa kuanzisha mjadala wa kuundwa kwa chombo kimoja
kitakachosimamia huduma za bima ya afya ili kuwafikia watanzania wote
katika utaratibu wa kuchangia kabla ya kuugua.
“Hadi
sasa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umeonesha mafanikio makubwa katika
utekelezaji wa majukumu yake ya kusimamia huduma za afya hali
inayonishawishi kuwa na chombo kimoja,” alisema Dk. Mwinyi.
Alisema
kuwa Serikali inatambua wingi wa mifumo na taasisi zinazojihusisha na
huduma za bima ya afya na lengo lililopo ni kuhuishwa ili kuimarisha
mfumo wa uchangiaji wa huduma za afya ambapo kwa sasa Mfuko wa Taifa wa
Bima ya Afya umekasimiwa mamlaka ya kuendesha Mfuko wa Afya ya Jamii
utakaoangalia namna nzuri ya kupanua wigo.
Akizungumzia
mchango wa NHIF katika uboreshaji wa huduma za matibabu vituoni,
alisema kuwa pamoja na juhudi zinazofanywa na Mfuko huo angependa kuona
Mfuko ukijikita katika uwekezaji unaolenga uboreshaji wa huduma za afya
na si vinginevyo, hivyo akaiagiza bodi mpya kuhakikisha inaagalia na
kuurejea upya utaratibu wa mikopo ya vifaa tiba na ukarabati wa majengo
ili watoa huduma wachangamkie zaidi fursa hiyo.
Dk.
Mwinyi pia hakusita kuzungumzia mahusiano mazuri ya kazi baina ya bodi,
menejimenti na watumishi wa Mfuko ambapo alisema kuwa Mfuko mpaka sasa
umefanikiwa kwa kiwango kikubwa kujenga misingi bora ya uhusiano mwema
wa kazi miongoni mwa watendaji wake ambao wamekuwa ni mfano wa kuigwa na
taasisi zingine hivyo akasisitiza hali hiyo kuendelezwa ili kuongeza
zaidi ufanisi wa utoaji huduma.
Naye
Kaimu Mkuu wa Wizara ya Afya, Regina Kikuli aliiambia bodi hiyo kuwa
jukumu walilokabidhiwa ni kubwa kwa kuwa linagusa moja kwa moja afya za
wanachama na watanzania kwa ujumla hivyo ni vyema bodi ikaliona hilo na
kuhakikisha inakuja na mbinu mpya za kuhakikisha inaimarisha na
kuboresha Mfuko huo ili uweze kufikisha malengo yake ya kuwahudumia
watanzania wote.
Kwa
upande wake Mwenyekiti mpya wa Bodi hiyo, Balozi Ali Mchumo aliahidi
kuwa kazi aliyokabidhiwa kwa kushirikiana na wajumbe wenzake wataifanya
kwa uaminifu mkubwa na kwa kutumia uwezo wao wote ili kuhakikisha Mfuko
huo unawasaidia watanzania wote.
Akitoa
maelezo ya utangulizi Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya, Emanuel Humba alisema kuwa moja ya mafanikio makubwa yaliyofikiwa
na Mfuko kwa sasa ni watanzania wengi kutambua umuhimu wa bima ya afya
hivyo Mfuko unafanya kila jitihada ya kuhakikisha inafikia watanzania
wengi zaidi na kukabiliana na changamoto zote zilizopo ili lengo la afya
bora kwa wote liweze kufikiwa.
No comments:
Post a Comment