Tanzania imetengeneza historia
mpya kwenye ngumi za kulipwa nchini Thailand baada ya mabondia wake kuwa
wanapigwa kila mara wanapokwenda kuiwakilisha nchi na bara la Afrika. Safari
hiiJEMBE, kijana mtanashati
anayeinukia kwenye masumbwi Jonas
Segu kutoka katika ukumbi wa mazoezi waRespect Gym Boxing Club ya Mabibo Loyola chini ya kocha Christopher Mzazi ameonyesha
kipaji kikubwa cha kusukuma msumbwi alipoushangaza umati wa maelfu ya wananchi
wa Thailand pamoja na
nchi za ukanda wa Indo-China.
Segu alikuwa anachuana na bingwa wa IBF katika mara la Asia
Pacific Patomsuk Pathompothong kutoka
Thailand katika uzito wa Light
Welter ambaye ni bondia namba 7 duniani katika viwango vya IBF. Mpambano wao
ulifanyika katika jiji lenye mahekalu ya dhahabu la Bangkok na kurushwa na television
katika nchi zote za ukanda wa Indo-Chinaza Laos,
Myanmar, Cambodia, Vietnam na Thailand yenyewe.
Mpambano wa Segu na Pathompothong ulianza kwa bondia
wa kitanzania kuchomoka kama upinde kwenye kona yake na kumshambulia Pathompothong kwa makonde mazito
ya kumshikisha adabu. Segu alitupa
makonde ya mchanganyiko na kumzidi Pathompothong kutokana
na uzito na umakini wa ngumi zake. Kwa kipindi chote cha raundi ya kwanza
ilimbidi Pathompothong ajilinde
na kukimbia akizunguka ndani ya ulingo ili kudhoofisha masumbwi yaSegu aliyekuwa anayachanganya
kama mashine ya kukomboa mpunga ambao unalimwa kwa wingi nchini Thailand!
Jonas Segu alikuwa chini ya
uangalizi makini wa bondia maarufu mstaafu George “Lister” Sabuni ambaye
aliweza kumpa maelekezo ya nini cha kufanya kwenye mpambano huo wa mwaka.
Katika raundi ya 2, 3 na 4 Segu aliuonyesha umati wa mashabiki wa
Thailand kuwa yeye kweli ni bingwa mtarajiwa na hakwenda Thailand kula wali wao
ila kuiwakilisha nchi yake ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Segu
alimhenyesha Pathompothong vilivyo kwa kumchakaza kwa makondde
mfululizo hususan akiutumia mkono wake hatari wa kulia ambao ulionekana dhahiri
kuwa unaleta madhara makubwa kwa Pathompothong.
Ilididi timu ya wataalam wa Pathompothong kutafakari namna ya
kumdhibiti kijana huyo wa Kitanzania ambaye kweli alionekana kuwa alienda
Thailand kuuchukua mkanda wa IBF
Pan Pacific na sio kufuata ulaji!
Raudi ta 5 Pathompothong aliingia
ulingoni akiwa mtu tofauti kabisa akirusha msumbwi mfululizo na kutembea
ulingoni kama siafu huku akimvuta Segu kenye kamba ili amkandamizie
masumbwi yake. Kijana huyo nadhifu wa kitanzania (mwenye sura nzuri ya kuvutia
na ambaye wasichana wengi wa Thailand walishinda karibu na hoteli aliyoshukia
ili kuweza kuongea naye) alitumia wakati huo kumwonyesha Pathompothong kuwa
yeye hababaishwi na masumbwi yake kwani amefanya
mazoezi ya kutosha. Segu alibadilishana masumbi na Pathompothong vilivyo na kuufanya umati wa mashabiki waliojazana kwenye
ukumbi huo kumshangilia kama vile yeye ndiye bondia wao wakiimba Tanzania,
Tanzania, Tanzania!
Katika
raundi ya 6 mabondia wote waliingia ulingoni kama vifaru na kubadilishana
masumbwi ya mchanganyiko (combinations) wakitafuta kudhibiti harakati za mpinzani
mwenza. Ni katika kubadilishana huku kwa masumbwi ambako Segu aliumizwa mkono
na Mthailand Pathompothong. Inawezekana kuwa ni katika juhudi
za kumzuia ili asiendelee kurusha masubwi ya nguvu na kudhoofisha nguvu zake.
Kuumia
mkono kwa Segu ilikuwa dhahiri kwani
mwanzoni mwa raundi ya saba wakati Pathompothong alipokuwa anamiliki ulingo dhidi ya kijana huyo mtanashati
wa kitanzania.
Katikati ya raundi ya saba Segu aliona
kuwa hawezi kuutumia mkono wake vizuri na kumwashiria refarii wa mpambano kuwa
anaacha!
No comments:
Post a Comment