Na Mwandishi Wetu
MAKAMU wa Rais Dk. Mohammed
Gharibu Bilal amesema Serikali iko tayari kushirikiana na Wasomi nchini katika
tafiti mbailimbali wanazofanya ili ziweze kuliletea Taifa maendeleo.
Akizungumza na wandishi wa
habari jijini Dar es Salaam, wakati wa ufunguzi wa maonesho ya nane ya Vyuo
Vikuu vya Elimu ya Juu, Dk. Bilal, alisema maonesho hayo yanalengo la kuonesha
juhudi zinazofanywa na vyuo hivyo.
Alisema lengo la serikali kufanya
hivyo ni kuona tafiti zinazofanywa na vyuo hivyo vinaleta tija katika kumaliza matatizo
yanayoikabili jamii.
“Nafurahi kuwa hapa
kushuhudia maendeleo yaliyofikiwa na vyuo
hususan katika elimu ya juu, sayansi na teknoloji”alisema Dk. Bilal.
Dk. Bilal alisema Mpango wa
maendeleo wa serikali wa miaka mitano ambao umezinduliwa mwaka 2011 na
kukamilika mwaka 2016 moja ya eneo inalolenga ni elimu ya ubunifu.
Aidha, serikali itaendelea
kuwekeza kwenye sekta ya elimu ya juu, siyansi na teknolojia ambapo pia
itashirikiana na sekta binafsi kwa ajili ya manufaa ya jamii.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa
‘Globle Education Link’ Abdulmalik Mollel, alisema wazazi wanapaswa kujiandaa
mapema katika kuwatafutia watoto wao nafasi za elimu ya juu mapema na si
kusubiri hadi watangaziwe matokeo ya kidato cha nne na sita.
Alitoa wito kwa wazazi
kuutumia mtandao wao ambao ni mahususi katika kuwatafutia wanafunzi vyuo vya
elimu ya juu vya ndani na nje ya nchi.
Mollel alisema hadi sasa
mtandao huo umefanikiwa katika kuwatafutia vyuo wanafunzi 700 hadi 800 tangu
ulipoanzishwa mwaka 2006.
No comments:
Post a Comment