Na Bryceson Mathias
PALIPO na upendo hapana uoga; naam, upendo kamili hufukuza Uoga wote. Basi, mtu mwenye uoga hajakamilika bado katika upendo, kwani uoga huhusikana na adhabu. Yohana 4:18.
Kama
kuna watu wanaoniudhi, basi ni wale ambao wanakumbatia dhambi na
kuipaka mafuta ing’ae, ambapo hata wakitaka kutubu, hawaitaji dhambi ila
wanasema wameteleza.
Dhambi
haina mlalahoi wala mlalahai, dhambi ni dhambi hata iwe ndogo au kubwa
bado inaitwa dhambi, na haiiitwi kuteleza, awe amefanya Rais au
Mwananchi!, Mfalme au Mtumwa wake.
Hivi
karibuni nilipate tabu moyoni, kuona Mwenyekiti wa Bunge na Mbunge wa
Peramiho Jenister Mhagama akimkatisha Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema)
Mchungaji Peter Msigwa, kutokana na kutumia maneno makali wakati
akichangia Hoja ya Mali Asili na Utalii.
Kosa
la Msigwa kukatishwa na Mhagama katika mchango wake, lilitokana na
awali kuanza kwa kuishambulia Ikulu ya Rais Kikwete ambayo ilitanguliwa
na Ma-Rais wengine, akiwemo Ally Hassan Mwinyi (Ruksa), na Benjamini
William Mkapa (Ukweli na Uwazi) dhidi ya Ujangili.
Msigwa
alikuwa akikosoa baadhi ya Makosa yalisababisha kuzalishwa na kukuzwa
kwa Mgogoro wa Loliondo, ambapo alimtuhumu Mwinyi kwamba aliuanzisha,
Mkapa aliupalilia, na kudai Kikwete anaulea.
Kabla sijasema lolote, ni rai yangu nimuulize maswali kadhaa Mwenyekiti Mhagama; Tusemeje basi? Tuendelee kutenda dhambi ili neema izidi kuongezeka? Hata kidogo! Itawezekanaje sisi tuliokufa kwa mambo ya dhambi, tuendelee tena kuishi humo? Rumi 6:1.
Hivi
karibuni Rais Kikwete katika hotuba zake za kila mwezi, aliliambia
Taifa hadharani kwamba, ‘Kuna misikiti mitatu mkoani Dar es Salaam,
imethubutu na kudiriki kumsomea Itikafu ili Afe! Binafsi niliposikia
nilishituka kama nimkatishe asiseme, lakini baadaye nililipenda tamko.
Nililipenda
tamko la Rais kwa sababu hakuwa muoga kulisema alikuwa wazi iliwatu
wajue, maana msema kweli ikiria, hata kama ni kibaya kwa wengine bila
kificho mbele ya watu hawi, mnafiki. Lakini wako wanafiki wanaosemea chini chini kwa kificho, hao ndio sio wazuri.
1Timotheo.5:8 “Lakini
mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake
hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini”
Nataka
kusema hivi, Msigwa anawapenda sana Viongozi wa Kitaifa wa Tanzania
pamoja na watu wao wanaowaongoza, ndiyo maana hataki kusema pembeni na
kuwa na uoga kama walivyo wengine, badala yake wanasengenya na kusema
ufichoni.
Mtu
akisema kwamba anampenda Mungu, hali anamchukia ndugu yake, huyo ni
mwongo. Maana mtu asiyempenda ndugu yake ambaye anamwona, hawezi
kumpenda Mungu ambaye hamwoni?.
Ni rai yangu kwa Wenyeviti wa Bunge akiwemo Mhagama waelewe, Palipo na upendo hapana uoga; naam, upendo kamili hufukuza Uoga wote. Basi, mtu mwenye uoga hajakamilika bado katika upendo, kwani uoga huhusikana na adhabu.
Kwa
uzoefu wa Jeshi muda mrefu, ninachofahamu mimi ni hiki, nidhamu ya Woga
ni kitu kibaya kwa Askari aliyeko medani. Wabunge ni Askari wa Mstari
wa Mbele kuwawakilisha wananchi katika haki na mustakabali wa maendeleo
yao.
Aidha katika hili ndiyo maana Biblia ikasema katika katika kitabu cha Pili cha Timotheo1:7 kwamba; “Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na yaupendo na ya moyo wa kiasi!.
Hivyo nawapenda sana wabunge wote wa Ushindani na wa Chama Tawala wanaoikosoa Serikali, wanaipenda nchi.
0715-933308
No comments:
Post a Comment