Katikati Redds Miss Kibaha Nzera Kitano , kushoto
mshindi wa pili Ester Albert na kulia ni Rachel Joh ambaye ni mshindi wa tatu.
Na Ripota Wetu, Kibaha
ALIYEKUWA mshiriki namba 6
katika shindano la kumsaka Redds Miss Kibaha 2013 Nzera Kitano ameibuka kua Redds Miss Kibaha 2013
katika shindano lililofanyika kwenye ukumbi wa Conteainer Kibaha Maili Moja mkoani Pwani Mei 17 mwaka
huu
Nzera ambae alionekana kuwa
mchezi tangu mwanzo wa shindano aliweza kupenya katika hatua ya nusu fainali
ambapo aliingia katika warembo watano bora kati ya washiriki 10 waliokuwa
wakishindana kuwania taji hilo.
Aidha kwa ushindi huo Nzera amepata zawadi ya fedha taslimu
sh.300,000 pia amepa ofa ya kwenda kuchagua vipodozi na mapambo ya aina
mbalimbali katika duka la Shear Illusion lilipo Mlimani City pamoja na
king’amuzi kutoka kampuni ya Multichoice ambapo atafungiwa bure.
Mshindi wa pili ni Ester
Albert ambaye amepata fedha taslimu kiasi cha sh.200,000 pia atapata ofa ya
kulipiwa ada ya shule au kutafutiwa kazi na mdau ambaye hataki kutaja kwenye
vyombo vya habari.
Mshindi wa tatu ni Rachel
John aliyepata fedha taslimu sh. 150,000 huku nafasi ya nne ikienda kwa Sylvia
John huku nafasi ya tano ilikwenda kwa Beatrice Bahaya.
Kwa ushindi huo warembo wote
watano wamepata nafasi ya kwenda kushiriki kwenye shindano la Redds Miss Pwani
watakakochuana na warembo wa Bagamoyo kuwania tiketi ya kwenda kushiriki katika
shindano la Kanda ikiwa ni katika kuwania tiketi ya shindano la taifa.
Shindano hilo limeandaliwa na
Kampuni ya Linda Media Solution (LIMSO) na kudhaminiwa na
Redds Miss Kibaha
ilidhaminiwa na Tanzania Distilleries Konyagi kupitia kinywaji cha Dododma
Wine, Redds Premium Cold, Fredito Entertainment, CXC Africa, Michuzi Media
Group |(MMG), Aco Catering & Servises, Pr Studio, ASET ,Santorine Holiday
Resort na Amazon Night Club.
Bendi ya Muziki wa dansi ya
Mashujaa ilitumbuiza na kuwachengua mashabi wa urembo wa mkoa wa Pwani.
No comments:
Post a Comment