Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, September 1, 2013

DIAMOND AMZAWADIA GARI GURUMO
HABARI/PICHA NA EVANCE NG'INGO
MSANII wa muziki wa kizazi kipya Nasib Abdul, Diamond  jana  alimkabidhi gari mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi nchini aliyestaafu muziki hivi karibuni, Muhidin Gurumo.

Diamond alimkabidhi mzee huyo gari hilo wakati wa hafla ya kuzindua video ya wimbo wake mpya uitwao My Number One iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
 Baada ya kuizungumzia video yake hiyo na changamoto aliyokutana nazo wakati wa kutengeneza video hiyo na ndipo alipomuita stejini mzee Gurumo na kuweka wazi  namna ambavyo amekuwa akimpenda na kumheshimu nguli huyo huku akisisitiza kuwa amesikitishwa na namna mzee huyo anavyohangaika kwa sasa.
Ndipo Diamond alipomuita jukwaani na kumkabidhi funguo wa gari hali iliyopelekea wageni waalikwa kupiga kelele za kushangilia baada ya kuguswa na tukio hilo.

Baada ya zoezi hilo, Diamond alimshika mkono mzee huyo na kisha wakiongozana na wageni waalikwa kwa pamoja walitoka nje na kwenda kuliangalia gari hilo kabla ya kurejea ndani na kuendelea na ratiba kama kawaida.
Akizungumzia Video yake hiyo alisema kuwa imemgharimu zaidi ya milioni 50 ambapo aliitengenezea nchini Afrika Kusini.
Ni Video nzuri na ya aina yake ambayo imegusa mazingira halisi ya maisha ambayo alikuwa akiyaimba katika wimbo wake huo wa mapenzi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...