Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, September 21, 2013

SIMBA USO KWA USO NA WABABE WA YANGA



LIGI Kuu ya Vodacom (VPL) inaingia raundi yake ya tano kesho (Septemba 21 mwaka huu) kwa mechi huku vinara Simba wakiwakaribisha Mbeya City kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Uwanja wa Mkwakwani, Tanga utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Mgambo Shooting Stars na Rhino Rangers ya Tabora. Mtibwa Sugar itakuwa mgeni wa Tanzania Prisons katika pambano litakalochezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Nayo Kagera Sugar itakuwa nyumbani kwenye uwanja wake wa Kaitaba mjini Bukoba kuvaana na Ashanti United ya Dar es Salaam katika mechi itakayochezeshwa na mwamuzi Jacob Adongo kutoka Mara.
Ligi hiyo itakamilisha mzunguko wa tano keshokutwa (Septemba 22 mwaka huu) kwa mechi tatu ambapo Azam na Yanga zitacheza Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam huku JKT Ruvu ikikwaruzana na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Azam Complex.
Ruvu Shooting inayokamata nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi itakuwa mgeni wa Coastal Union katika mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Wakati huo huo, Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inaendelea wikiendi hii kwa mechi kumi na moja. Kundi A kesho (Septemba 21 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Transit Camp na Green Warriors (Uwanja wa Karume, Dar es Salaam), Tessema na African Lyon (Uwanja wa Mabatini, Mlandizi).
Ndanda itacheza na Villa Squad kwenye Nangwanda Sijaona mjini Mtwara wakati keshokutwa (Septembe 22 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Polisi Dar es Salaam na Friends Rangers katika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Kundi B kesho (Septemba 21 mwaka huu) ni Mkamba Rangers dhidi ya Burkina Faso kwenye Uwanja wa CCM Mkamba, na Mlale JKT itakuwa mwenyeji wa Kurugenzi Mafinga kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea. Keshokutwa (Septemba 22 mwaka huu) ni Majimaji na Kimondo katika Uwanja wa Majimaji.
Mechi za kundi C kesho (Septemba 21 mwaka huu) ni Pamba dhidi ya Polisi Dodoma (Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza), Stand United na Polisi Tabora (Uwanja wa Kambarage, Shinyanga) na Kanembwa JKT itacheza na Mwadui kwenye Uwanja wa Kawawa ulioko Ujiji. Keshokutwa (Septemba 22 mwaka huu) Polisi Mara na Toto Africans zitacheza Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...