Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, September 14, 2013

DAR FILAMU FESTIVAL INAMTAMBULISHA LULU KWENUTAMASHA Kubwa la Filamu litakaloandika historia ya tasnia ya filamu Tanzania la Dar Filamu Festival (DFF 2013) linamtambulisha Elizabeth Michael kama Official Actress for DFF 2013/14 katika muonekano mpya akiwa kama balozi wetu wa kwanza kutambulishwa kutoka DFF, alafu utapata muonekano wa Official Director/ Producer DFF 2013/2014 Vincent Kigosi ‘Ray the Greatest’.
Dar Filamu Festival 2013 awali ilitambulishwa kwa wadau na wanahabari wiki iliyopita na sasa tupo katika hatua nyingine ya kuwatangaza na kuwapa majukumu mabalozi wetu ambao ni Ray na Lulu katika kuhakikisha kampeni ya kupenda filamu za Kiswahili na kuzipa thamani zinafanikiwa na kuwa ni soko lenye nguvu zaidi katika tasnia ya filamu Ulimwenguni.
Tamasha la Dar Filamu Festival (DFF 2013) litafanyika katika viwanja vya CoICT- UDSM- Kijitonyama kuanzia tarehe 24 hadi 26 Septemba 2013, filamu za Kitanzania kama ufunguzi wa tamasha hilo zitaonyeshwa kwa kiingilio cha Bure kabisa  kiingilio chako ni kufika katika viwanja vya Posta pale Kijitonyama na kushuhudia filamu kutoka kwa wakali wa filamu Bongo Movie.
Sasa ni zamu yako kukutana na Lulu kisha kuongea naye kuhusu filamu na soko jipya la Filamu,  kupitia Projector kubwa  na kuona filamu kwa uzuri zaidi huku ukiburudika kwa kazi nzuri kutoka nyumbani.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...