Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, September 16, 2013

PPRISCA CLEMENT ATWAA TAHI LA REDD'S MISS TANZANIA TALENT 2013


Mrembo Prsica Clement, kutoka Kitongoji cha Sinza (katikati) akipunga mkono kwa furaha baada ya kutangazwa mshindi wa shindano la Redd's Miss Talent kwa mwaka 2013, na kufanikiwa kupata tiketi ya kuingia hatua ya 15 bora ya shindano la Redd's miss Tz mwaka huu.
Washiriki wa shindano la kumtafuta mshiriki wa kuingia katika hatua ya 15 bora ya Shindano la Redd's Miss Tanzania kwenye shindano la Redd's miss tz Talent 2013 wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutangazwa washindi wa hatua ya tano bora.
***********************************************
Na Mwandishi Wetu
WAKATI homa ya shindano la Redd’s Miss Tanzania ikiwa inapanda kwa washiriki wote, mrembo Prsica Clement juzi usiku alifanikiwa kutwaa taji la Redd’s Miss Tanzania Talent lililofanyika katika hoteli ya Giraffe iliyopo Kunduchi, Dar es Salaam.
 
Kutokana na ushindi huo, Prisca ambaye anatokea Sinza akiwakilisha Kanda ya Kinondoni, amefanikiwa kuingia katika hatua ya 15 Bora ya Redd’s Miss Tanzania.
 
Majaji wa shindano hilo walilazimika kumpa ushindi Prsica kutokana na uhodari wake wa kucheza na moto, hivyo kuwashinda washiriki wote 30 wa shindano hilo.
 
Watazamaji wengi waliofurika katika ukumbi wa hoteli hiyo, walikubaliana na uamuzi wa majaji wa kumpa ushindi huo.
 
Shindano la Redd’s Miss Tanzania linatarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Mlimani City, uliopo Mwenge, Dar es Salaam ambapo mshindi ataondoka na gari dogo lenye thamani ya Sh milioni 15 na kitita taslimu cha fedha cha Sh milioni 8.
 
Mbali na mshindi kutwaa zawadi hizo, mshindi wa pili atapata Sh milioni 6.2, mshindi wa tatu Sh milioni , mshindi wa nne Sh milioni 3, mshindi wa tano Sh milioni 2, mshindi wa sita hadi 15 atapata Sh milioni 1.2 na waliobaki watapata Sh 700,000 kila mmoja.
 
Akizungumzia ushindi huo, Prsica alisema hiyo ni dalili njema kwake ya kutwaa taji hilo na ana uhakika mkubwa atafanikiwa kuwa mshindi.
 
Naye Meneja wa Redd’s Original, Victoria Kimaro alisema, shindano la mwaka huu limekuwa na msisimko mkubwa zaidi kutokana na washiriki wote kuwa na sifa zinazolingana.
 
“Mwaka huu Redd’s Miss Tanzania imepata washiriki bomba zaidi na naamini litakuwa na ushindani mkubwa na wa aina yake,” alisema Victoria.
 
Taji la Redd’s Miss Tanzania kwa sasa linashikiliwa na Brigitte Alfred aliyelitwaa taji hilo mwaka jana na kukabidhiwa gari aina ya Noah pamoja na kitita cha Sh milioni 8.
 
Shindano la Redd’s Miss Tanzania linadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...