Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, September 14, 2013

TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 FUNIKA BOVU NDANI YA DODOMA


Mkongwe wa muziki wa kizaz kipya a.k.a Bongofleva Afande Sele a.k.a Baba Tunda  a.k.a Simba Mzee akidhihirisha ukongwe juu ya steji ya tamasha la
Serengeti linalofanyika usiku huu ndani ya uwanja wa Jamuhuri mkoani
Dodoma,ambapo maelfu ya watu washabiki wamejitokeza kushuhudia tamasha  hilo ambalo hufanyika mara moja kwa mwaka.
 Msanii mahiri ambaye kwa sasa anasumbua vilivyo anga ya muziki wa
Bongofleva,Diamond akiwaimbisha mashabiki wake usiku huu kwenye tamasha  la serengeti fiesta 2013,linalofanyika usiku huu kwenye uwanja wa
Jamuhuri.
Haaaa haaaa...ukitaka kubana pua kabane nyumbani kwenu,hapa ni hip hop
tuuu.....Msanii wa Bongofleva Ney wa Mitego wakioneshana umahiri umwamba wa jukwaani na msanii mwenzake  Dimond  kupitia wimbo wa Muziki Gani.
Maelfu ya Watu wakiwa kwenye uwanja wa jamuhuri,usiku huu wakishangweka na tamasha la Serengeti Fiesta 2013.
 Mwanadada ambaye wengi wanadai amerithi viuno na sauti kutoka mwanamuziki Ray C,anaitwa Rachael kutoka nyumba ya vipaji a.k.a THT akiimba jukwaani huku akionesha umahiri wake wa kukata mauno.
PICHA ZAIDI  INGIA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...