Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, September 14, 2013

BEN POL AIPUA 'WAUBANI'
Na Elizabeth John
MKALI wa muziki wa RnB nchini, Bernad Paul ‘Ben Pol’, anajipanga kuachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Waubani’ ambao amemshirikisha chipukizi wa muziki huo, Alice ikiwa ni muendelezo wa kuwapa burudani mashabiki wake.Ben Pol alishawahi kutamba na vibao vyake kama ‘Pete’, ‘Maneno’, ‘Samboila’, ‘Yatakwisha’ na nyinginezo ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri katika tasnia ya muziki huo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Ben Pol alisema yuko katika hatua za mwisho za uandaaji wa kazi hiyo, ambayo anatarajia kuisambaza mwanzoni mwa wiki ijayo.

Mkali huyo amewaomba wapenzi wake wakae mkao wa kula kwa ajili ya kazi hiyo, ambayo anaamini itafanya vizuri kutokana na ubora wa mashairi yaliyo ndani yake.


“Wapenzi wa kazi zangu waendelee kunipa sapoti katika kazi zangu kama hapo awali kwani kuna vitu vizuri ambavyo nimewaandalia, hivyo wategemee vitu adimu kutoka kwangu,” alisema Ben Pol.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...