Mfungaji
nyota wa timu ya Utumishi, Anna Msulwa akifunga goli huku mchezaji wa
Taswa Queens, Elizabeth Mbassa akiwa hana la kufanya katika mchezo
uliofanyika kwenye uwanja wa Leaders Club. Utumishi ilishinda kwa mabao
43-19 Utumishi yaigalagaza Taswa queens magoli 43-19.
*************************************
Na Mwandishi Wetu
BAADA
ya kutamba kwa muda mrefu bila kufungwa, timu ya netiboli ya waandishi
wa habari za michezo nchini (Taswa Quuens) juzi ilichezea kichapo kikali
cha mabao 43-19 kutoka kwa timu ya Utumishi katika mchezo wa kirafiki
uliofanyika kwenye uwanja wa Leaders Club.
Taswa
Queens ambao ni mabingwa wa Tamasha la Waandishi wa Habari la Arusha,
haikuwi kufungwa tokea kuanzisha kwake mwezi Aprili mwaka huu.
Katika
mchezo huo, Taswa Queens ilianza kwa kasi kupitia wafungaji wake,
Zainabu Ramadhan na Imani Makongoro na kufunga 3-0 katika dakika za
mwanzoni kabla ya Utumishi kutumia mfungaji wake nyota, Anna Msulwa (GA)
kubadili kibao na kuanza kuisambaratisha Taswa Queens.
Msulwa
ambaye alikuwa nyota wa mchezo, alionyesha uwezo mkubwa akishirikiana
na GS wake, Fatuma Machenga na kuweza kuongoza kwa mabao 22-10 hadi
mapumziko.
Taswa
Queens iliweza kucheza vizuri pamoja na kichapo hicho na kutokuwepo kwa
mchezaji wake, Sharifa Mustafa kulisababisha timu hiyo kutoweza kucheza
vizuri.
Utumishi
iliwatumia wachezaji wake nyota ambao wanatamba katika mchezo wa
netiboli nchini kama Amina Ahmed ambaye pia anachezea Don Bosco kwa
upande wa mpira wa kikapu, Elizabeth Fusi, Sharon Batenga, Monica Aloyce
na Zaujia Abdallah.
Akizungumza
baada ya mchezo huo, Msulwa alisema kuwa mchezo huo ulikuwa wa
maandalizi kwa ajili ya michezo ya Shimiwi na wamefarijika kuvunja mwiko
wa Taswa Queens kwa kutofungwa.
“Taswa
Queens ni timu nzuri na inaweza kufikia hatua kubwa zaidi kama itaweza
kuongeza bidii, kwa Utumishi ni ishara tosha ya kufanya vyema katika
michezo ya Shimiwi,” alisema Msulwa.
No comments:
Post a Comment