Mchezaji
Said Maulid aliyejiunga na Ashanti United akitokea nchini Angola msimu
huu amepata ITC ambayo sasa inamwezesha kuchezea timu hiyo katika mechi
za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inayoingia mzunguko wake wa tatu keshokutwa
(Septemba 14 mwaka huu).
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa
(ITC) kwa Watanzania wawili kucheza mpira wa miguu nchini Afrika Kusini.
Wachezaji
hao; Robert Kobelo na Mohamed Ibrahim wamepewa hati hizo baada ya
kuombewa na Chama cha Mpira wa Miguu Afrika Kusini (SAFA) kama wachezaji
wa ridhaa ili wajiunge na klabu ya Cacau United ambayo timu yake
inacheza Ligi Daraja la Pili katika Wilaya ya Cacau.
No comments:
Post a Comment