Cheka alifanikiwa kutwaa ubingwa huo wa
dunia baada ya kumchakaza kwa pointi aliyekuwa akiushikilia ubingwa huo,
Mmarekani Phil Williams katika pambano lililopigwa kwenye Ukumbi wa Diamond
Jubilee, Upanga jijini Dar, Agosti 30, mwaka huu.
Cheka alipewa viwanja hivyo kwa nyakati
tofauti mkoani Morogoro ambapo kimoja kipo Segera, Mvomero na kingine kipo
Morogoro mjini.
Joel Bendera ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa
Morogoro, alimkabidhi Cheka kiwanja kilichopo Morogoro mjini chenye thamani ya
shilingi milioni sita kwa niaba ya manispaa ya mkoa huo huku wananchi wa mkoani
humo wakiahidi kumjengea nyumba kwenye kiwanja hicho.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Cheka
alisema amefurahia zawadi hiyo na amejisikia faraja kuona serikali inatambua umuhimu
wake.
“Nashukuru sana kwa kweli kwa viwanja hivi, kimoja
kipo Segera, Mvomero, bado sijakiona ila hiki kingine cha mjini tayari
nimeshakabidhiwa hati na kila kitu,” alisema Cheka.
No comments:
Post a Comment