Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, September 3, 2013

WASANII WA BONGO MOVIE WAIPONGEZA KAMPUNI YA PROIN PROMOTIONS KWA UZINDUZI WA FILAMU YA LULU IITWAYO FOOLISH AGE NA KULETA USHINDANI


Uzinduzi wa filamu ya Foolish Age ambayo waigizaji wakuu ni Elizabeth Michael(Lulu), Diana Kimaro, Ombeni Phir, Jengua na Hashim Kambi ulifanyika wikiend iliyopita Mlimani City, Dar es salaam, na kuwa na mafanikio kwa watu na mastaa wa filamu kuhudhuria vizuri. Mastaa kadhaa walizungumza na Swahiliworldplanet na kutoa maoni yao juu ya uzinduzi huo na kampuni ya Proin Promotions kwa ujumla iliyofanikisha uzinduzi huo ambayo pia ni kampuni mpya inayojihusisha na usambazaji wa filamu Swahiliwood. Maoni ya baadhi ya mastaa wa filamu kuhusu uzinduzi huo ni haya hapa chini.............

Shamsa Ford: Kwa upande wangu kila kitu kilikuwa sawa, pia ni faraja kwetu wasanii kuona wasambazaji wanaongezeka.

Slim Omar: Kwa upande wangu nimejifunza kwasababu ni kitu kipya na kama mapungufu basi ni kawaida katika jambo lolote, lakini kwa kweli ni mwanzo mzuri sana na wa kujifunza kwa wasambazaji na wadau wote wa filamu Tanzania, nawapongeza sana waliofanikisha ni jambo zuri na la kuigwa.

Nice Mohamed(Mtunisy): Sikuwepo hivyo ni ngumu kutoa maoni.

Efranciah Mangii: Uzinduzi ni mzuri na umefana tunachohitaji ni mafanikio kwa sisi wasanii kutokana na kazi zetu tunazozifanya, kampuni za usambazaji zipo japo hazitoshi wasanii tunaongezeka daily kutokana na hilo wasambazaji wamekuwa wakiwalipa wasanii pesa kidogo zisizokizi mahitaji ya msanii kwa Proin Promotions wamefanya kitu kizuri iwe mfano kwa kampuni nyingine za usambazaji ili kujua thamani ya msanii na kazi zake.

Yobnesh Yusuph(Batuli): Kwanza nampongeza sana Lulu, unapokuwa kioo cha jamii watu wengi wanakuangalia aidha kwa ubaya au kwa uzuri na kwa mapito aliyopitia Lulu kila mtu alitegemea hakuna jipya tena kutoka kwake lakini imekuwa sivyo alinyoosha mikono yake juu na mungu ni mwema akatenda miujiza kwake. Nampongeza sana kwa jitihada zake, namuomba awe mpya kabisa kampuni ya Proin imemfanyia uzinduzi wa heshima na hadhi kubwa. Lulu ajitambue na akubali kuwa amekuwa sasa sio mtoto tena, aonyeshe makubwa zaidi na ajilinde na scandals zisizo na lazima, achague pa kwenda hasa kwa weekend na aangalie  kampani alizonazo. Shule ni muhimu na azidishe taaluma yake, atambue ana marafiki na maadui pia namtakia kila la kheri.

Nawapongeza Proin Promotions pia kwa kuguswa na matatizo yetu na hatimae wameamua kuwekeza kwenye tasnia hii ya filamu, naomba management ya Proin Promotions isiangalie majina ya watu ndiyo wafanye nao kazi waangalie vipaji vya watu bila kujali madaraja kwamba huyu star au upcoming wawe tofauti na makampuni yaliyopo, wawe na tuzo kwa waliofanya vizuri kila mwisho wa mwaka na wasisikilize wasanii wanafiki watakaoenda kuwaponda wengine au kuwaharibia wenzao.

Rachel Haule:  Kiukweli mimi nimefurahi sana hasa kwa sisi ma-producer ni fursa nyingne na nzuri kwetu si unajua tena wasanii wote tunamtegemea muhindi tu! yaani binafsi namuomba mungu amsaidie huyu msambazaji ni imani akisimama atazidi kuleta mwanga kwa ma-producer.Na Treem Salim

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...