Mwenyekiti
wa Makampuni ya Proin, Bw Johnson Lukaza akitoa neno kwa wadau
waliojitokeza kushuhudia fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents
(TMT) lililokuwa pia likirushwa live kupitia Kituo Cha Runinga cha ITV
Mwanaafa
Mwinzago (katikati) akishangilia Mara baada ya kutangazwa Mshindi wa
Kitita Cha Milioni 50 za Kitanzania katika Fainali ya Kumsaka Mshindi wa
Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 lililofanyika usiku wa
kuamkia leo katika Ukumbi wa Mlimani City na Kuhudhuriwa na Mamia ya
Watanzania.
Mwanaafa
Mwinzago (katikati) akiwa katika picha ya Pamoja na wazazi wake na timu
ya wafanyakazi wa TMT na washiriki wenzie mara baada ya kukabidhiwa
mfano wa Hundi ya Shilingi Milioni 50 za Kitanzania Mara baada ya
Kuwabwaga Washiriki wenzie tisa na Kuibuka Mshindi wa Kitita Cha Milioni
50 za Kitanzania katika Fainali ya Kusaka Vipaji Vya Kuigiza Nchini
lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents (TMT) ambalo limefikia Ukingoni
Jana Katika Ukumbi wa Mlimani City.
Washiriki wa Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 waliofanikiwa kuingia Kumi Bora wakiwa wanasubiri mshindi atangazwe
Host
Wa TMT 2014 Joti akimpongeza Baba wa Mwanaafa Mwizago kwa Mwanae kuibuka
Mshindi wa Fainali ya Tanzania Movie Talents (TMT) na kuibuka na kitita
cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania
Mwanaafa
Akiwa amembeba Mdogo wake mara baada ya kutangazwa Mshindi wa Fainali
ya Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 na kuibuka na kitita cha Shilingi
milioni 50.
Lulu
akionyesha Bahasha iliyokuwa na JIna la Mshindi wa Tanzania Movie
Talents (TMT) ambae ni Mwanaafa Mwinzago na Kumfanya kujishindia
Shilingi Milioni 50 za Kitanzania
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar waliojitokeza kushuhudia fainali ya TMT ambayo ilikua ikirushwa live kupitia ITV.