Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, August 25, 2014

Madini Migodini yapo Salama- Maswi

1.  Meneja wa Kampuni ya TANCOAL  (wanne kulia) Tan Brereton  na  Mkuu wa Masoko wa kampuni hiyo Emmanuel Constantinides (wa tatu kulia) wakimwonesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi  na ujumbe wake namna shughuli za himbaji Makaa ya Mawe zinavyofanyika.

 Gari la kubeba kupakia Makaa ya Mawe likiendelea na kazi hiyo katika Mgodi wa Ngaka unaomilikiwa na kampuni TANCOAL.
 Mashine ya kusaga makaa yam awe katika viwango mbalimbali kulingana na mahitaji ya wateja ikiendelea na kazi ya kusaga mawe katika Mgodi wa Mkaa ya Mawe wa Ngaka unaomilikiwa kwa ubia na Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) na kampuni ya Australia.
  Gari la kubeba makaa ya Mawe katika mgodi wa Ngaka likimwaga makaa sehemu maalum kutoka mgodini kabla ya kusagwa katika viwango mbalimbali kulingana na mahitaji y wateja.
 
=======  ========  ======
Madini Migodini yapo Salama- Maswi
Ø Aeleza TMAA wapo kuhakiki   mwenendo wa uzalishaji,uuzaji
Ø Mwekezaji  asisitiza Makaa ya Ngaka yana ubora wa juu
Na Asteria Muhozya, Mbinga
Katibu Mkuu  wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi amewataka watanzania kuondoa dhana kuwa madini  yanayochimbwa katika migodi mbalimbali nchini yanaibwa  na wawekezaji wakubwa na kusisitiza kuwa, Wizara  kupitia Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), wapo katika migodi yote nchini kuhakikisha kwamba madini hayo hayatoroshwi .
Maswi  ameyasema hayo alipotembelea Mgodi wa kuchimba Makaa ya Mawe  wa kampuni ya  Tancoal eneo la Ngaka wilayani Mbinga inayomilikiwa kwa ubia kati ya Kampuni ya Australia na Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) na kuongeza kuwa, TMAA wapo katika kila mgodi  kujua kiasi cha madini kinachochimbwa, kinachouzwa na kwa  ajili ya kuhakiki vyeti vya mauzo ya madini hayo kuhakikisha kuwa vinakwenda sambamba na kiasi cha mrahaba kinachotolewa na wawekezaji.
Kwa upande wake Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Paul Masanja alisisitiza hoja ya Katibu Mkuu Maswi na kuongeza kuwa, Wizara kupitia maafisa wa TMAA wamekuwa wakifanya ukaguzi kuhakikisha kwamba serikali inapata mrahaba stahili kupitia madini yanayouzwa na kutoa mfano kwa madini ya Makaa ya Mawe ya Ngaka kwamba serikali inapata asilimia 100 ya mrahaba.
“Nawapongeza sana TanCoal ni wasikivu, maafisa wa TMAA huwa wanafanya ukaguzi kila baada ya miezi mitatu kujua kiasi kinachozalishwa na kinachouzwa hivyo, tunakwenda nao vizuri,” alisisitiza Masanja.
Naye  Mkurugenzi wa Tancoal  Tan Brereton ameeleza kuwa,  mgodi wa wa Ngaka ni mradi mkubwa kwa Tanzania na kuongeza kuwa, uwepo wa mgodi wa makaa ya mawe wa Tancoal ni mafanikio na maendeleo makubwa kwa Tanzania kutokana na  kuwezesha ajira kwa wataalamu mbalimbali nchini ikiwemo serikali kupata kodi na mirahaba kupitia mgodi huo jambo ambalo litawezesha kuboresha huduma za kijamii.
Aidha, amezitaja faida  za nyingine za mgodi huo kuwa, uwepo wa Mgodi huo utawezesha Tanzania kuzalisha kiasi kikubwa cha nishati ya umeme kutokana na uwepo wa kiasi kikubwa cha makaa hayo katika mgodi wa Ngaka  na kueleza kuwa, makaa ya mawe kutoka katika mgodi huo yana ubora wa kiwango cha juu tofauti na madini yanayochimbwa nchini Afrika Kusini.
“Makaa ya Ngaka yana ubora wa hali ya juu sana tofauti na makaa ya nayochimbwa Afrika Kusini kwasasabu madini haya hayahitaji kusafishwa kabla ya matumizi tofauti na mengine ambayo husafishwa kabla ya kutumiwa ,alisisitiza Tan.
Aidha ameongeza kuwa,  kampuni hiyo ina uwezo wa kuzalisha kiasi cha tani  480,000  za makaa ya mawe kwa mwaka na kuongeza kuwa, tayari kampuni hiyo imesaidia huduma mbalimbali za kijamii katika maeneo ya afya,shule ,maji na kuwaendeleza vijana na kutumia zaidi ya shilingi milioni mia sita na kuongeza kuwa, kampuni hiyo imekwisha toa kiasi za bilioni 2 kama kodi na mrahaba  kwa serikali.
Kwa mujibu wa Tan, ameeleza kuwa, makaa yanayozalishwa na kampuni hiyo yanatumika katika viwanda vya  saruji vya Mbeya Tanga Lake,  kampuni ya METL na viwanda vya karatasi viwanda vya nguo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...