Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, August 7, 2014

RAIS BUSH AMSIFIA MAMA KIKWETE KUTOKANA NA JITIHADA ANAZOZIFANYA ZA KUHAMASISHA WANAWAKE KUPIMA UGONJWA WA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI


IMG_6232 
Na Anna Nkinda – Maelezo, Washington
Rais wa zamani wa Marekani George W. Bush amempongeza Mke wa Rais Mama Kikwete kutokana na kazi nzuri anayoifanya ya kuhamasisha jamii na wanawake kwa ujumla kujitokeza kwa ajili ya kupima saratani ya matiti na mlango wa kizazi.Pongezi hizo zilitolewa jana na Rais huyo mstaafu ambaye pia ni mwanzilishi wa Taasisi ya George W. Bush wakati akifungua mkutano wa wake wa Marais wa Afrika uliofanyika katika ukumbi wa  mikutano uliopo kituo cha  Kennedy (Kennedy Center) kilichopo mjini Washington.Mzee Bush alisema Taasisi yake inasimamia mradi wa upimaji wa saratani ya matiti na mlango wa kizazi, ili nchi za Afrika ziweze  kupunguza idadi ya wanawake wanaosumbuliwa na ugonjwa huo na hadi sasa zaidi ya wanawake 100000 wamefanyiwa uchunguzi katika nchi za Tanzania, Zambia na Botswana lakini tatizo lililopo ni unyanyapaa kwa  wagonjwa  wanaukutwa na tatizo hilo.

Alisema uchunguzi huo umefanyika kwa kipindi cha miaka mitatu kwani saratani ya mlango wa kizazi ni moja kati ya magonjwa makubwa yanayoua wanawake wengi katika nchi zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara  kwakuwa wanawake wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi (VVU) wako katika hatari kubwa zaidi ya kuugua ugonjwa huo.
Taasisi ya George W. Bush inafadhili mradi wa Utepe wa Pinki Utepe Mwekundu (PRRR) ambao ndiyo wasimamizi wa mradi huo uliogharibu zaidi ya  dola za kimarekani milioni mbili ambao pia utazinduliwa hivi karibuni katika nchi za Namibia na Ethiopia na zikufanya nchi zinazofadhiliwa kufikia tano.
“Tatizo kubwa ni Ujinga , upatikanaji wa taarifa zisizo sahihi na unyanyapaa vinazuia  maendeleo ya  afya ya jamii na hivyo wanawake kushindwa kwenda kupata chanjo ya kuzuia ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi (Human Papilloma Virus Vaccine) lakini watu wengi wanakufa kutokana na unyanyapaa ambao uko juu.  Naamini unaweza kuvunjwa mara moja kama  kioo”, alisema Mzee Bush.
Aliwahimiza wake hao wa Marais kuungana kwa pamoja ili kuweza kuimarisha afya ya mama na wasichana  kwani njia moja ya kuwasaidia watoto ni kuwasaidia mama zao.  Na kusisistiza kwamba ni jambo la muhimu kwa watu wanaoishi na VVU kutokufa  kwa magonjwa yanayoweza kutibika na kuzuilika.
Kwa upande wake Mke wa Rais wa Marekani Mama Michelle Obama alisema wake wa Marais wa Afrika wana kazi kubwa ya kuzisaidia jamii zao kutokana na matatizo yanayowakabili kwani  wanawake wengi na watoto wanakabiliwa na changamoto mbalimbali hasa za afya na elimu.
Kwa upande wa  vijana alisema wanafanya kazi sana katika jamii lakini bado wanakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo za ugonjwa wa Ukimwi.  Wao kama viongozi wanatakiwa kuhakikisha kuwa matatizo yao  yanatatuliwa.
“Tunaweza kuwakusanya watu hawa  katika meza moja ili kuweza kutatua changamoto zao, nyie ni sauti za wanyonge wakiwemo wanawake na watoto jitahidini kuwafikia wanawake wengi zaidi.
Wakati tunatoa kipaumbele kwa wasichana wetu tunakazi kubwa ya kufanya naamini majadiliano haya yatatoa jitihada mpya na nini cha kufanya ili tuweze kuwasaidia vijana wetu, ” alisema Mama Obama.
Mama Salma Kikwete ni mmoja wa wake wa Marais wa Afrika waliohudhuria mkutano huo uliandaliwa na Mke wa Rais wa Marekani Mama Michelle Obama kwa kushirikiana na Taasisi ya George W. Bush  ambao ulijadili uwekezaji katika elimu,  upatikanaji wa afya ya wanawake na wasichana na kuimarisha mahusiano kati ya sekta za umma na binafsi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...