Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, August 20, 2014

Alhaj Ali Hassan Mwinyi asema bado viongozi wanatumia madaraka yao kujinufaisha


Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi (katikati) akifungua semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma. Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi (katikati) akifungua semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi akifungua semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma. 
Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi akifungua semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Salome Suzete Kaganda (kwanza kushoto) akizungumza kwenye semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma. Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Salome Suzete Kaganda (kwanza kushoto) akizungumza kwenye semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.

Baadhi ya washiriki katika semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma. Baadhi ya washiriki katika semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma. Baadhi ya washiriki katika semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.Baadhi ya washiriki katika semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma. Baadhi ya washiriki katika semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.Katibu Msaidizi Kanda ya Mashariki, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Getrude Cyriacus (wa kwanza kushoto) akiwasilisha mada juu ya Rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma kwa wanasemina. Katibu Msaidizi Kanda ya Mashariki, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Getrude Cyriacus (wa kwanza kushoto) akiwasilisha mada juu ya Rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma kwa wanasemina. Baadhi ya washiriki katika semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.


Na Joachim Mushi, Dar

RAIS Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi amesema bado viongozi wa umma wanatumia madaraka yao na Ofisi zao kwa kujinufaisha wenyewe na kuwasahau wananchi waliowaweka madarakani hivyo kuna kila sababu ya kuleta sheria ya kuziba mianya hiyo kwa viongozi wanaokwenda kinyume na maadili.

Alhaj Mwinyi ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua semina ya majadiliano kati ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na wanahabari waliojadili rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.

Alisema licha ya kuwepo kwa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995 inayotumika sasa bado kumekuwa na wimbi kubwa la mienendo ya matumizi mabaya ya ofisi na madaraka kwa viongozi wa umma kwa kujinufaisha wenyewe kimaslahi.

"...Maana yake ni kwamba umma sasa haupewi kipaumbele unavyo stahiki. Maamuzi ya viongozi yanatolewa kwa maslahi binafsi na hivyo kudhihirisha kuwepo kwa tatizo la mgongano wa maslahi. Viongozi hao waliopewa dhamana na wananchi wanatumia rasilimali za umma ili kujinufaisha binafsi au shughuli zao ambazo wanazo pembeni," alisema Rais huyo mstaafu.

Alisema hata hivyo sheria ya maadili ya viongozi wa umma imekuwa na mapungufu kwa kuwabana baadhi ya viongozi wa umma na kuwaacha wengine pamoja na watumishi wa umma hivyo kujikuta nao wakijihusisha na mgongano wa kimaslahi.

Hata hivyo, ameongeza kuwa tayari Serikali imeona mianya hiyo na hivyo kuanza mchakato wa kuja na sheria maalum itakayo dhibiti hali hiyo. "...Nadhani mmewahi kusikia mara kwa mara namna ambavyo Rais wetu Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiagiza Serikali kufanya jitihada za dhati ili kuhakikisha kuwa viongozi wa umma wanaacha au wanajiepusha na tabia ya kushiriki zaidi kwenye biashara na kuacha jukumu lao...," alifafanua Mwinyi akiwaeleza washiriki wa semina hiyo.

Aidha aliipongeza Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa kuanza mchakato wa kutungwa kwa sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma, ambapo itakapo kamilika huenda ikawa suluhisho la mgongano wa kimaslahi kwa viongozi na watumishi wa umma.

Rais huyo mstaafu aliwataka wanasemina kuijadili rasimu iliyowasilishwa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na kutoa maoni yao kuiboresha zaidi ili itoke na majibu ya kero ya muda mrefu ya Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma.

Kwa upande wake, Katibu Msaidizi Kanda ya Mashariki, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Getrude Cyriacus akiwasilisha mada juu ya Rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma kwa wanasemina kabla ya mjadala alisema wataalam wa Sekretarieti hiyo wamefanya utafiti kwenye mataifa mbalimbali na kutoka na mapendekezo ambayo yataongoza mjadala kuelekea kupata sheria nzuri.

Naye Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Salome Suzete Kaganda akizungumza katika semina hiyo, alisema Rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma walioiandaa itajadiliwa na wadau mbalimbali ili kupata maoni kabla ya kuwasilishwa kwenye baraza la makatibu wakuu kuboreshwa zaidi kabla ya mchakato kupanda ngazi za juu.

Aidha aliwataka wananchi na wadau wengine kuendelea kuijadili Rasimu ya Sheria Mpya ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi kwa Viongozi wa umma pindi itakapo wafikia na kutoa maoni kwa lengo la kuiboresha zaidi ili itakapo kamilika iweze kufanya kazi vizuri na kujibu kero zilizopo katika eneo hilo la viongozi wa umma.

“...Mapendekezo ya sheria hii hayalengi kuwafanya viongozi kuwa maskini, bali kasi yao ya ukwasi iendane na hali halisi ya kipato chao. Sheria hii itakapopitishwa itapunguza ubinafsi wa viongozi walioko madarakani kujipendelea wenyewe na maeneo wanayotoka.” Alifafanua Jaji Kaganda.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...