Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, August 30, 2014

BONDIA THOMAS MASHALI KUMKABILA HENRY WANDERA WA KENYA OKTOBA 4 TANDALE



 Bondia Thomas Mashali katikati akisaini mkataba wa kucheza na Henry Wandera kutoka Kenya oktoba 4 katika ukumbi wa New Madiba 'Korini' uliopo Tandale Dar es salaam wanaoshudia kushoto ni Raisi wa oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO, Yassini Abdallah 'Ostadhi' na promota wa mpambano huo Khamis Ally picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
 Rais wa TPBO Yassin Abdala akiandika mkataba wa bondia Thomas Mashali katikati atakaepambana na mkenya Henry Wandera oktoba 4 katika ukumbi wa New Madiba 'Korini' uliopo Tandale Dar es salaam kulia ni  promota wa mpambano huo Khamis Ally picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Thomas Mashali katikati akisaini mkataba wa kucheza na Henry Wandera kutoka Kenya oktoba 4 katika ukumbi wa New Madiba 'Korini' uliopo Tandale Dar es salaam wanaoshudia kushoto ni Raisi wa oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO, Yassini Abdallah 'Ostadhi' na promota wa mpambano huo Khamis Ally picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Na Mwandishi Wetu

BONDIA Thomas Mashali 'Simba asiyefugika' anatarajia kupanda uringoni tena  oktoba 4 mwaka huu kumvaa mkenya Henry Wandera mpambano utakaofanyika katika ukumbi wa New Madiba zamani Korini

Mashali anapigana uku akiwa na historia ya kupoteza mpambano wake wa mwisho zidi ya bondia Mada Maugo ambapo walicheza katika uwanja wa taifa na kupoteza kwa point mpambano huo

akizungumzia mpambano huo Mashali amesema atokubali kupoteza tena mchezo huuo ukizingatia anachezea nyumbani kwao alopozaliwa na ndipo alipoanzia ngumi maeneo ya Tandale hivyo sito kubali niaibike mbele ya ndugu zangu hivyo nawambia wapenzi waje kwa wingi kuangalia mashali anavyofanya kazi yake ya mchezo wa masumbwi

nae promota wa mpambano huo Khamis Ally amewahakikishia kuwa sehemu ya parkingi ni kubwa na ulinzi ni wa kutosha kifupi katika ulinzi tumejipanga vizuri pia siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine mazuri ya utangulizi ambapo mabondia wengi wamejitokeza kucheza siku hiyo

siku hiyo pia kutakuwa na huuzwaji wa 
DVD ambazo zinatoa mwanga kwa mchezaji kujua mchezo na kufahamu zaidi mbinu mpya zitumiwazo na mataifa mbali mbali Duniani.

Wakiwemo mabondia bingwa wa dunia kama Manny Paquaio,Floyd Maywether,Amir Khani, Mohamed Ali ,Mike Tayson na wengine wengi wanaotamba na waliotamba katika mchezo huo wa masumbwi Duniani
kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ametoa wito kwa makampuni mbalimbali kujitokeza kutoa sapoti ya mchezo wa masumbwi kwani ndio mchezo pekee unaoweza kututoa kimasomaso watanzania tukafurahi

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...