Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, August 6, 2014

MKUU WA MKOA WA KATAVI ATEMBELEA BANDA LA MBEYA YETU NANE NANE AMWAGA SIFA KEM KEM.

Banda la Mbeya yetu Blog
Mtoa Maelezo kutoka Tone Multimedia Group kupitia Mtandao wao wa Mbeya yetu Blog Fredy Anthony Njeje wa kwanza kulia akitoa maelezo ya kina kwa   Mkuu wa Mkoa wa  katavi  Mh.Dr Rajab Lutengwe jinsi mtandao wa Mbeya yetu unavyofanya kazi pia unavyosaidia upatikanaji wa habari kwa urahisi kabisa. Pia kuekeza sababu za Kushiriki katika mashindano ya nane nane ikiwa ni pamoja na Kutoa elimu juu ya mitandao ya kijamii na faida zake hasa upande wa Blogs na matumizi sahihi.

  Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh.Dr Rajab Lutengwe akiwapongeza Tone Multimedia Group kwa kuanzisha Mtandao wa Blogs za Mikoa na Mbeya yetu Blog ikiwemo ndani yake kwa ubunifu mkubwa na kazi kubwa wanayoifanya ili kufikisha taarifa kwa kila mkoa na Mtandao wake na kusisitiza kuwa ni vizuri kuendelea na moyo huo huo ili kuendelea kuhabarisha jamii kwa ujumla.
  Mkuu wa Mkoa wa Katavi  Mh.Dr Rajabu Lutengwe  wa tatu kutoka kushoto akitoa ushauri kwa Blog ya katavi yetu baada ya kuweka Mnyama Tembo awekwe mnyama Kiboko kwa sababu ndiye alama kubwa ya utalii katika Mbuga ya Wanyama ya Katavi.
 Fredy Anthony Njeje akiendelea kumpa maelezo Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr. Rajab Lutengwe juu ya kazi zengine ambazo kampuni ya Tone Multimedia Group inazifanya ikiwa ni pamoja na Radio ya Mtandaoni Tone Radio, Mtandao Maalum ambao unawahusu wanafunzi Matukio na wanavyuo, Huduma Mpya ya kupata habari kwa njia ya Simu kwa watu wenye Whatsapp Tone Mobile News, Mtandao wa watanzania waishio nje ya nchi pamoja na kazi zote za ambazo kampuni inazifanya. Wa kwanza kutoka kushoto ni Mwandishi wa Mbeya yetu Venance Matinya.
Mwandishi Mkuu wa Mbeya yetu Blog Joseph Mwaisango wa kwanza upande wa kushoto akiendelea kutia maelezo kwa baadhi ya watu waliotembelea katika banda la Mbeya yetu blog.
************
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr. Rajab Lutengwe, ameusifia mtandao wa kijamii wa Mbeya Yetu Unaomilikiwa na Tone Multimedia Group kwa kuonesha mabadaliko ya kwenda na wakati katika  teknolojia ya  mawasiliano na habari teknolojia ya kisasa.

 Dr. Lutengwe ametoa pongezi hizo hivi wakati akitoa tathmini yake mara baada ya kutembelea mabanda mbalimbali kwenye maonesho ya wakulima  maarufu kama Nane nane yanayoendelea kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

Alisema kuwa mtandao huu umeonesha chachu ya mabadaliko katika sekta ya mawasiliano kwa kukuza na kutangaza uchumi wa ndani na nje ya nchi kwa kurusha matukio mbalimbali yanayoendelea katika maonesho hayo.

“Nimewapenda sana wale vijana wa mtandao wa Mbeya Yetu  kwa kazi yao ya kurusha matukio yanayoendelea kwenye viwanja hivi, huko tunakoelekea hivi sasa katika kukuza biashara ya mazao yetu ni lazima tutangaze kupitia ‘Google’ Mbeya yetu imeonesha njia sahihihi ya kukabiliana na soko la uchumi na kama wataenedelea na kasi ile watafika mbali” alisema.

Alisema kwa kutumia mitandao ya kijamii taarifa mbalimbali zinazohusu sekta ya kilimo zinawafikia wananchi wengi kwa mara moja na kuwa ni muhimu kwa halmshauri za wilaya kuanzisha Tovuti na Blogu ili kuendana na wakati.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...