Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, August 30, 2014

MABONDIA CHEKA NA SHAURI KUZIPIGA AUGOST 30 JAMUHURI MOROGORO

Mabondia Ramadhani Shauri na Cosmas Cheka wakitunishiana misuli
  Na Mwandishi Wetu

Mabondia Ramadhani Shauri na Cosmas Cheka watazipiga tena mwishoni mwa mwezi huu Augost 30 katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro akizungumzia mpambano huo bondia Shauri amesema kuwa yupo fiti ingawa katika mechi yake ya mwisho aliyocheza nje ya nchi alipa cuting katika jicho la kulia ata hivya ata hakikisha anafanya vizuri katika mpambano huo

utakaofanyika Morogoro nae mratibu wa mpambano huo Kaike Siraju amesema maandalizi yote ya mpambano huo yameshakamilika kinachosubiliwa ni siku tu ya mpambano huo tu aliongeza kuwa katika mpambano huo kutakuwa na mapambano ya utangulizi yatakayowakutanisha mabondia 

Twaha Kiduku atakaezipiga na Deo Njiku wakati Juma fundi atazipiga na Epson John na mapambano merngine ya utangulizi

siku hiyo pia kutakuwa na huuzwaji wa 
DVD ambazo zinatoa mwanga kwa mchezaji kujua mchezo na kufahamu zaidi mbinu mpya zitumiwazo na mataifa mbali mbali Duniani.

Wakiwemo mabondia bingwa wa dunia kama Manny Paquaio,Floyd Maywether,Amir Khani, Mohamed Ali ,Mike Tayson na wengine wengi wanaotamba na waliotamba katika mchezo huo wa masumbwi Duniani
kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ametoa wito kwa makampuni mbalimbali kujitokeza kutoa sapoti ya mchezo wa masumbwi kwani ndio mchezo pekee unaoweza kututoa kimasomaso watanzania tukafurahi

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...