Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, March 12, 2015

MAYWEATHER NA PAQUAIO WAKUTANISHWA KWA MARA YA KWANZALAS VEGAS, Marekani

TIKETI ya bei ya chini katika pambano la ngumi za kulipwa kati ya Floyd Mayweather pamoja na Manny Pacquiao zinapatikana kwa pauni 1,000 (sh mil 2.7.
 
Mabondia hao wanatarajia kupanda ulingoni Mei 2 mwaka huu katika Ukumbi wa GMG Las Vegas katika pambano linalosubiriwa kwa hamu na mashabiki na wapenzi wengi wa mchezo huo ulimwenguni.

Katika pambano hilo tiketi za kuzunguka katika ulingo zinatarajiwa kuuzwa kwa pauni 5,000 kwa tiketi sawa na sh. Milioni 13.5.

Pambano hilo ndilo linatarajiwa kuwa la ghali na la historia zaidi kuliko mapambano yoye yaliyopita.

Juzi mabondia hao walikutana kwa mara ya kwanza kwa ajili ya kuzungumza na waandishi wa Habari juu ya pambano hilo.

Pacquiao alisema kuwa anashukuru Mungu kutokana na kufikia mpaka siku hiyo, ambapo anatarajia kuwapa raha mashabiki wake ambayo walikuwa wanaisubiri kwa kipindi cha miaka mitano sasa.


Mayweather alisema kuwa pambano hilo linatarajiwa kuwa la kipekee na ndio pambano bora zaidi kwake tofauti na mapambano 47 aliyowahi kucheza ambapo hana historia ya kupoteza hata moja.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...