Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, October 22, 2015

BONDIA LULU KAYAGE AZIDI KUJIFUA KWA AJILI YA MAPAMBANO YA KITAIFA NA KIMATAIFA


Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' akimnowa bondia Lulu Kayage wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa na mpambano wake wa kugombania mkanda wa taifa desemba 25 na bondia Mwanne Haji mpambano utakaofanyika mkoa wa Morogoro katika uwanja wa jamuhuri picha na SUPER D BOXING NEWSBONDIA LULU KAYAGE
Bondia Lulu Kayage kushoto akielekezwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D'  jinsi ya kupiga ngumi za mkunjo wa chini 'upcut' ambazo zinapigwa mbavuni Kayage anajiandaa na mipambano yake mbalimbali ya kitaifa na ya kimataifa picha na SUPER D BOXING NEWS
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' akimnowa bondia Lulu Kayage wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa na mpambano wake wa kugombania mkanda wa taifa desemba 25 na bondia Mwanne Haji mpambano utakaofanyika mkoa wa Morogoro katika uwanja wa jamuhuri picha na SUPER D BOXING NEWS

Na Mwandishi Wetu

BONDIA wa kike Lulu Kayage ameingia kambini kwa ajili ya mapambano yake ya kimataifa na kitaifa yatakayo mkabili siku za usoni bondia huyo ambaye ana uchu wa kufika mbali katika mchezo wa masumbwi nchini

ambapo Desemba 25 ata pambana na bondia Mwanne Haji kugombania ubingwa wa taifa katika mpambano wa raundi kumi utakao fanyika katika uwanja wa jamuhuri Morogoro

bondia huyo aliye onesha hudhubutu wa kumtwanga Winnie Mphahlele wa Afrika ya kusini mpambano uliofanyika Town Hall, katika mji wa Limpopo, South Africa kwa T.K.O ya raundi ya tatu kwenye mpambano wa raundi sita amekuwa tishio katika ukanda wa afrika na anataka kudhilisha kuwa yeye ni zaidi ya mabondia wengine

bondia huyo anaenolewa na jopo la makocha likiongozwa na Habibu Kinyogoli 'Masta' uku kocha na mshauli wa karibu wa bondia huyo akiwa ni Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye anaratibu mapambano mbalimbali ya bondia huyo ndani na nje ya nchi

Kayage ametamba kumsambalatisha mwanne Haji kama alivyo mfanya mkaburu wakati wa mpambano wake uliofanyika agost 9 uko afrika ya kusini na kuendeleza ubabe wake

na kocha Rajabu Mhamila 'Super D' aliongeza kwa kusema Lulu ana moyo wa mazoezi na anajituma hivyo watanzania watambue wamepata mwokozi atakaeleta furaha katika mioyo yao na kuipeperusha vema bendera ya taifa nchini kwa kuwa nia anayo uwezo anawo


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...