Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, October 17, 2015

BONDIA VICENT MBILINYI AMPIGIA MIKWALA DEO NJIKU KUPAMBANA DESEMBA 25


BONDIA VICENT MBILINYI


Na Mwandishi Wetu

BONDIA Vicent Mbilinyi amesaini mkataba wa kuzipiga na Deo Njiku wa Morogoro siku ya Desemba 25 katika uwanja wa jamuhuri morogo wakisindikiza mpambano wa Fransic Cheka na Thomasi Mashali mpambano uho wa raundi sita

utakuwa wa kwanza kwa bondia Mbilinyi kucheza mkoa wa morogoro akizungumzia mpambano huo bondia huyo amesema kuwa anamjua mpinzani wake vizuri kutokana na ukongwe wake kwa kuwa alianza zamani kupigana ata hivyo mimi nina jiamini na nitamkalisha katika raundi za awali

bondia huyo alieweka kambi yake mkoa wa pwani maeneo ya Kibaha ambapo ameweka kambi yake kwa ajili ya mpambano huo
bondia huyo anaefundishwa na Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi ncini Rajabu Mhamila 'Super D' amejizatiti kumtwanga vizuri tu Deo njiku ili ajisafishie njia ya kuwa bingwa wa mchezo wa masumbwinchini
nae Kocha wake Rajabu Mhamila 'Super D;' aliongeza kwa kusema kuwa ana matumaini na bondia wake kwa kuwa na rekodi nzuri ya mchezo ambapo mpaka sasa amecheza michezo 7 kashinda 5 droo 1 na kupoteza 1 kwa rekodi hiyo bondia huyo ana uchu wa kubaki kileleni na kuendeleza kichapo kwa kila bondia anaekutana nae

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...