Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, March 21, 2016

MABONDIA KUPIMA UZITO MANGO GARDENI JUMAMOSI KWA AJILI YA KUCHEZA MARCH 27 JUMAPILI YA PASAKANa Mwandishi Wetu

MABONDIA waendelea kutambiana kuelekea mpambano wao wa Pasaka march 27 uwanja wa ndani wa Taifa Dar es salaam 

akizungumzia mpambano uho mratibu wa pambano hilo Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa mabondia wote wapo tayali kwa kuwa wapo na afya tele na wanaendelea na mazoezi yao ya mwisho mwisho kila mmoja akijitamba kumsambalatisha mwenzake 

ambapo mabondia mahasimu Fransic Miyeyusho na Nassibu Ramadhani wanakutana kwa mara nyingine kwa ajili ya mpambano wao mwingine baada ya ule wa mwanzo Miyeyusho kuibuka Mbabe

mpambano mwingine mkali utakuwa ni kati ya bondia Mada Maugo na Abdallah Pazi ambao wametafutana kwa mda mrefu na sasa wamaliza ubishi siku ya jumapili hii ya march 27 katika uwanja wa ndani wa taifa

Super D aliongeza kwa kusema mabondia wote watapima uzito siku ya jumamosi pale katika ukumbi wa Mango Garden Kinondoni  na mpambano utafanyika jumapili ya Pasaka Matrch 27 uwanja wa ndani wa Taifa

'Super D' aliongeza kwa kusema kuwa mipambano hiyo inayosubiliwa kwa hamu na mashabiki lukuki
 
 kutakuwa na mipambano ya kukata na shoka mingine bondia  

 Pius Kazaula atakumbana na Seba Temba mpambano mwingine utawakutanisha Cosmas Cheka na Mohamed Matumla
 
Katika mpambano uho kutakuwa na uhuzwaji wa vifaa vya mchezo wa ngumi pamoja na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kwa ajili ya kutambua sheria mbalimbali za mchezo zitakazokuwa zikitolewa bule kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa galama nafuu

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...