Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, March 1, 2016

NGUMI KUPIGWA BAGAMOYO MARCH 5 UKUMBI WA TASUBA


Na Mwandishi Wetu

BONDIA Seba Temba wa kg 66 kutoka mkoa wa Morogoro anatarajia kupanda ulingoni march 5 katika ukumbi wa Tasuba Bagamoyo kupambana na mkali wa mkoa huo wa Pwani Iddi Pialali mpambano uho ambao umeandaliwa na Muhsin Sharif 

promota huyo alisema kuwa siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine mengi ya mchezo wa ngumi likiwemo la wanawake Joyce Awino kg 64  na Mariam Tembo na Abdallah Pazi kg 76 atakumbana na Georger Dimoso na Flank Lampad kg 69 atavaana na Mwaite Juma wakati bondia kutoka mkoa wa Tanga Jacobo Mganga kg 72

atapambana na Maono Ally

mpambano uho ni rasmi kabisa kwa ajili ya kutoa burudani kwa wakazi wa Bagamoyo mkoa wa Pwani pamoja na vitongoji vyake ambao walikuwa wakisubili burudani hiyo ya mchezo wa masumbwi nchini

nae bondia Seba Temba amejinasibu kwa kujigamba lazima amlaze Iddi Pialali na ndio itakayokuwa njia yake ya mazoezi kabla ya kupambana na bondia Pius Kazaula mpambano utakaofanyika march 27 katika uwanja wa ndani wa taifa siku ya sikukuu ya Pasaka

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile

Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...