Marquee
tangazo
Tuesday, January 3, 2012
BREAKING NEWS: MADAKTARI WA HOSPITAL YA TAIFA MUHIMBILI WAANZA MGOMO LEO
ASHA BARAKA AHUDHURIA PATI YA URBAN PULSE NA MISS JESTINA GEORGE LONDON
Mkurugenzi wa ASET Club na Bendi ya African Stars 'Twanga pepeta', Asha Baraka (kushoto) akiwa na Miss Justina George, ikiwa ni ishara ya kuuaga mwaka 2011 na kuukaribisha mwaka 2012, 2akati wa sherehe hiyo iliyofanyika Jumamosi iliyopita ndani ya kiota kipya cha maraha The Pit Stop 'Uwanja wa Nyumbani'.
Urban Pulse Creative na Miss Jestina George Blog wanapenda kuwashukuru wadau wote waliojitokeza kuja siku ya Jumamosi iliyopita kusherekea kwa pamoja ndani ya kiota kipya cha maraha The Pit Stop 'Uwanja wa Nyumbani' bila ya kumsahau mkurugenzi wa ASET Asha Baraka katika party ya kuuga mwaka 2011 na kuukaribisha mwaka 2012 hapa jijini London.
Mdau,Frank wa Urban Pulse, akisherekea Mwaka Mpya na Wadau wengine ukumbini humo.
Wadau wakijumuika kwa pamoja kuukaribisha mwaka mpya na kuuaga mwaka 2011.
Wadau, walimbwende wakila pozi wakati wakipata kujisevia flani ukumbini humo.
RAIS KIKWETE AOMBOLEZA VIFO VYA AZIZ SHEWEEN NA BALOZI ATHUMAN MHINA
Rais Jakaya Kikwete, akiweka sahihi kwenye kitabu cha maombolezo ya kifo cha Aziz Sheween, Mikocheni jijini Dar es salaam, Jumatatu jioni nyumbani kwa marehemu Ofisa huyo wa Mambo ya Nje Mkuu Daraja la kwanza katika Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, aliyefariki dunia huko Riyadh, Saudi Arabia.
Rais Kikwete akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezo alipofika Madale jijini Dar es salaam, jana Jumatatu jioni nyumbani kwa Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Balozi Athumani Mhina aliyefariki dunia usiku wa kuamkia jana alipokuwa akipelekwa katika Hospitali ya Jeshi Lugalo kutibiwa shinikizo la damu.
Rais Kikwete, akiagana na baadhi ya wanafamilia ya marehemu ya Aziz Sheween, baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu huyo Ofisa Mambo ya Nje Mkuu Daraja la I katika Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, aliyefairiki juzi huko Riyadh, Saudi Arabia.
Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuia ya Wazazi ya CCM,
Balozi Athumani Mhina enzi za uhai wake.
KATIBU Mkuu wa Jumuia hiyo, Khamis Dadi alisema Balozi Mhina alifariki usiku wa kuamkia jana aliokuwa akipelekwa katika Hospitali ya Jeshi Lugalo kutibiwa shinikizo la damu.
Dadi alisema Mhina alikuwa akipelekwa hospitali baada ya hali yake kubadilika ghafla kutokana na maradhi ya shinikizo la damu.Alisema mwili wa marehemu, ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM, umehifadhiwa katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo na kwamba mazishi yake yanatarajiwa kufanyika kesho.
Monday, January 2, 2012
KONYAGI watoa msaada kwa wahanga wa Mafuriko.Kikundi cha Konyagi Cocioty chaonyesha ukakamavu ktk kugawa misaada!!
Diamond aswekwa rumande Iringa
MSANII maarufu wa muziki wa kizazi kipya Naseeb Abdul a.k.a Diamond na wacheza show wake wawili wamejikuta wakifunga mwaka vibaya baada ya kutupwa rumande kwa kosa la kumshambulia na kuharibu mali za mwandishi wa habari wa mkoani Iringa Francis Godwin.
Sakata la Diamond kumshambulia mwanahabari huyo maarufu hapa nchini lilitokana na hatua utata uliokuwa umejitokeza katia uwanja wa Samora mjini Iringa ambako Diamond alipaswa kufanya onyesho lake ya kuuanga na kuukaribisha mwaka 2012 .
Hata hivyo onyesho hilo lilionyesa kuwa na kila aina ya utapeli baada ya ratiba kuonyesha kuanza saa 8 mchana na kumalizika mida ya saa 12 za jioni na baada ya hapo uwanja huo ulipaswa kutumiwa na umoja wa Makanisa mkoani Iringa kwa ajili ya mkesha wa kufunga mwaka na mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt Christina Ishengoma ndie alikuwa mgeni rasimi.
HIvyo kutokana na msanii huyo kushindwa kuonekana hadi mida ya saa 11.50 jioni mashabiki kiduchu ambao walikuwa wameingia katika uwanja huo walilazimika kumvaa mmoja kati ya wahusika katika onyesho hilo ambaye alikuwa akichukua fedha za kiingilio mlangoni na kuanza kuhoji sababu ya onyesho hilo kukwama na msanii Diamond na Afande Sele ambao walipaswa kupagawisha kutoonekana hadi mida hiyo na kuhoji sababu ya tiketi za chama cha soka mkoa wa Dar e s Salaam (DRFA) ambazo zinaonyesha kuna mchezo wa kirafiki kati ya Asante Kotoko ya Ghana na Marafiki wa Uhuru mchezo uliochezwa 12/11/2011 uwanja wa Taifa na kiingilia ni shilingi 5000 huku wao wamefika kuona wasanii na sio mechi.
Hata hivyo haikuchukua muda ghafla Costa ambayo ilikuwa imembeba Diamond na wacheza show wake bila Afande Sele iliwasili uwanjani hapo na kufanya mashabiki kupunguza jazba.
Kutokana na hali ya utulivu kurejea uwanjani hapo mwandishi wa habari huyo ambaye ni mmiliki wa blogu maarufu nchini ya www.francisgodwin.blogspot.com
Sakata la Diamond kumshambulia mwanahabari huyo maarufu hapa nchini lilitokana na hatua utata uliokuwa umejitokeza katia uwanja wa Samora mjini Iringa ambako Diamond alipaswa kufanya onyesho lake ya kuuanga na kuukaribisha mwaka 2012 .
Hata hivyo onyesho hilo lilionyesa kuwa na kila aina ya utapeli baada ya ratiba kuonyesha kuanza saa 8 mchana na kumalizika mida ya saa 12 za jioni na baada ya hapo uwanja huo ulipaswa kutumiwa na umoja wa Makanisa mkoani Iringa kwa ajili ya mkesha wa kufunga mwaka na mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt Christina Ishengoma ndie alikuwa mgeni rasimi.
HIvyo kutokana na msanii huyo kushindwa kuonekana hadi mida ya saa 11.50 jioni mashabiki kiduchu ambao walikuwa wameingia katika uwanja huo walilazimika kumvaa mmoja kati ya wahusika katika onyesho hilo ambaye alikuwa akichukua fedha za kiingilio mlangoni na kuanza kuhoji sababu ya onyesho hilo kukwama na msanii Diamond na Afande Sele ambao walipaswa kupagawisha kutoonekana hadi mida hiyo na kuhoji sababu ya tiketi za chama cha soka mkoa wa Dar e s Salaam (DRFA) ambazo zinaonyesha kuna mchezo wa kirafiki kati ya Asante Kotoko ya Ghana na Marafiki wa Uhuru mchezo uliochezwa 12/11/2011 uwanja wa Taifa na kiingilia ni shilingi 5000 huku wao wamefika kuona wasanii na sio mechi.
Hata hivyo haikuchukua muda ghafla Costa ambayo ilikuwa imembeba Diamond na wacheza show wake bila Afande Sele iliwasili uwanjani hapo na kufanya mashabiki kupunguza jazba.
Kutokana na hali ya utulivu kurejea uwanjani hapo mwandishi wa habari huyo ambaye ni mmiliki wa blogu maarufu nchini ya www.francisgodwin.blogspot.com
Baada ya hapo mashabiki walimlazimisha Diamond kupanda jukwaani kuimba vinginevyo wangemchapa hivyo kulazimika kupanda jukwaani huku akisimamiwa kwa bakora na mawe ,pamoja na kupanda jukwaani bado alishindwa kuimba baada ya wale waliokodisha vifaa vya muziki kugoma kupiga muziki kwa madai muda wao umekwisha huku watu wa mkesha wa makanisa nao wakipinga jukwaa la ibada ya mkesha kutumika kwa mambo ya kidunia hali iliyozua utata . Hali hiyo ilimfanya Diamond kuchanganyikiwa zaidi na kushindwa kushuka jukwaani kwa kuhofia kichapo toka kwa mashabiki kutokana na hali hiyo mwandishi alianza kufanya mahojiano na kuchukua picha za mashabiki kusubiri na kumsimamia msanii huyo kabla ya kuruka jukwaani na kikosi chake na kuanza kumchapa mwandishi huyo ambaye pia alionyesha kukabiliana nao kwa kiasi na kusaidiwa na mashabiki . Kutokana na tukio hilo mwandishi huyo wa habari Godwin alipoteza camera yake yenye thamani ya shilingi milioni 1.5, simu moja yenye thamani ya shilingi 300,000 huku Laptop yake ndogo aina ya Acer ikiharibiwa na msanii huyo. Tukio hilo lilifikishwa polisi na Diamond kufunguliwa mashtaka ya kushambulia kwa RB namba IR/RB/ 7700/2011 na baada ya muda mida ya saa 1.30 usiku jeshi la polisi lilikwenda kumkamata msanii huyo na vijana wake wawili ambao walikuwa katika Hotel ya Staff Inn Anex mjini hapa wakijipumzisha na kupelekwa mahabusu hadi asubuhi . Mratibu wa show hiyo Mike T akiomba msamaha kwa mwandishi huyo alisema kuwa msafara wa Diamond ulikuwa ukitokea Mbeya katika uwanja wa Sokoine ambako pia Show ilikwama kutokana na mvua kubwa kunyesha na baada ya hapo walianza safari kwa ajili ya kuja Iringa na kukwama kufika kwa wakati kutokana na basi lao la kwanza kuharibika na kulazimika kukodi Costa na kufika kwa mida mibaya Iringa na kuwa baada ya Iringa Msafara huo ulitaraji kwenda jijini Dar es Salaam kuzindua Albam yake . |
SIMU YA MCHINA YAMLIPUKIA NA KUMUUNGUZA HAULE
Mbunge wa Jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe (kulia) akimjulia hali mfanyabiashara wa mafuta katika Kijiji cha Luilo Ludewa, Joseph Haule ambaye amelipuliwa na mafuta baada ya simu yake ya kichina kulipuka,majeruhi huyo anatibiwa katika Hospital ya Wilaya ya Ludewa, mkoani Iringa. (PICHA ZOTE NA FRANCIS GODWIN)
Filikunjombe na baadhi ya wananchi wakimjulia hali Joseph Haule
Joseph Haule akiwa amelazwa Hospitali
Filikunjombe na baadhi ya wananchi wakimjulia hali Joseph Haule
Joseph Haule akiwa amelazwa Hospitali
MDAU WA WWW.ELIMUBORA.COM AMALIZA KOZI YA WEB DESIGN
Evance ambae anaratibu website ya www.elimubora.com akiwa anapokea cheti baada ya kuhitimu kozi fupi nchini India. Amewataka watanzania hususan wadau wa masuala ya IT kufuatilia udhamini mbalimbali wa kozi fupi utolewao na chuo hicho kwa taarifa zaidi ingia katika libeneke lake la www.elimubora.com
RAIS JAKAYA AWAAPISHA MAKATIBU WAKUU WAWILI NA NAIBU KATIBU MKUU MMOJA IKULU DAR LEO
Rais Jakaya Kikwete aklimwapisha Mh Eliakim C. Maswi kuwa Katibu Mkuu wizara ya Nishati na Madini katika hafla iliyofanyika Iukulu leo jijini Dar es salaam. (PICHA NA IKULU)
Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, akimpongeza na kumkabidhi zawadi ya ua Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Eliackim Chacha, baada ya kuapishwa leo Ikulu Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu Ikulu, Susan Paul, Katibu Mkuu Ikulu, Peter Alanambula Ilomo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliackim Chacha, kabla ya kuapishwa wakati Makamu akiingia katika Ukumbi huo kwa ajili ya kuhudhuria hafla ya kuapishwa kwa makatibu hao walipokuwa wakisubiri kuapishwa rasmi kushika nafasi hizo Ikulu Dar es Salaam leo Januari 2, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Rais Jakaya Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja na Naibu wake, Adam Malima, Katibu Mkuu wa wizara hiyo aliyeapishwa leo Januari 2, 2012, Ikulu Dar es Salaam pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Wizara hiyo baada ya kuapishwa Katibu huyo. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Rais Dk. Jakaya Kikwete wa pili wa tatu kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa rais Dk. Gharib Bilal wa pili kutoka kushoto na makatibu walioapishwa leo kutoka kulia ni Mh Peter Ilomo Katibu Mkuu Ikulu, Naibu Katibu Mkuu Ikulu Mh Suzana Mlawi,Balozi Ombeni Sefue katibu mkuu kiongozi na mwisho kushoto ni Mh Eliakim C. Maswi Katibu Mkuu wizara ya Nishati na Madini PICHA NA IKULU MATUMLA AMGALAGAZA CHEKA KWA POINTI
Saturday, December 31, 2011
RAIS KIKWETE, LEO AMUAPISHA BALOZI SEFUE KUWA KATIBU MKUU KIONGOZI, BADALA YA LUHANJO
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha rasmi, Balozi Ombeni Yohana Sefue, kuwa Katibu Mkuu Kiongozi badala ya Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Phillemon Luhanjo, aliyemaliza muda wake. Hafla hiyo ya kumuapisha Balozi Sefue, imefanyika leo Ikulu Dar es Salaam. Wa pili (kushoto) kwa Rais ni Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Phllemon Luhanjo, akisimamia zoezi hilo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiingia katika ukumbi wakati wa hafla fupi ya kumuapisha Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana Sefue, aliyeapishwa na Rais Jakaya Kikwete, Ikulu Dar es Salaam leo.
KATIBU Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana Sefue, ni Manataaluma ya Dipromasia ambaye tokea Agosti 31, 2010, amekuwa mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Jijini New York, Marekani.Kabla ya kuteuliwa kwenda kuwa mwakilishi wa Umoja wa Mataifa, Balozi Sefue, alikuwa ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani katika mji wa Washington DC tokea Juni 15, 2007. Na kabla ya hapo alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada, nafasi aliyoishikilia tangu Oktoba 2005 hadi Juni 2007.
Sefue, pia amewahi kuwa Ofisa Mwandamizi katika Ubalozi wa Tanzania nchini Sweden katika Mji wa Stockholm kati ya mwaka 1987 na 1992.![]() |
Miongozni mwa mambo mengine, Balozi Sefue alimsaidia Rais Mkapa wakati alipikuwa Kamishna wa Afrika (kwenye Kamisheni ya Waziri Mkuu wa Uingereza wakati huo, akiwa ni Tony Blair), ambapo alitoa ripoti iitwayo, ‘Our Common Interest, Ripoti of the Commission for Africa’, mwezi Machi mwaka 2005, na pia alishiriki kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi za G8, ambao ulijadili ripoti hiyo ambao ulifanyika Gleneagles, Scotland mwezi Julai mkwa 2005.
Aidha Balozi Sefue, alifanya kazi na Rais Mkapa wakati Mheshimiwa Mkapa alipokuwa Mwenyekiti mwenza wa Kamisheni ya Shirika la Kazi Duniani ya ILO World Commission, iliyojadili masuala ya Kijamii ya Utandawazi kati ya mwaka 2002 na 2004, ambapo alishiriki katika maandalizi ya ripoti ya Kamisheni hiyo iitwayo, A Fair Globalisation Creating Opportunities For All, iliyotolewa mwzi Februari mwaka 2004.
Balozi Sefue, alipata Elimu yake ya Juu katika Chuo Kikuu cha Mzumbe (ambacho kwa sasa ni Chuo Kikuu cha Mzumbe) katika masuala ya Utawala mwaka 1997.
Pia alipata Shahada ya Uzamili katika masuala ya Sera na Utawala kutoka Institute of Social Studies (ISS) mjini The Hague, Uholanzi mwaka 1981.
Alipata Diploma ya Juu katika Chuo cha Diploma cha Dar es Salaam mnamo mwaka 1986, na pia Balozi Sefue alimuoa Mama Anita M. Sefue na anawatoto wawili. Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana Sefue, wakipiga picha ya pamoja baada ya hafla ya kuapishwa rasmi kwa katibu huyo leo Ikulu Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana Sefue na Balozi Kiongozi Mstaafu, Phillemon Luhanjo, wakizungumza jambo baada ya hafla ya kuapishwa rasmi kwa katibu huyo leo Ikulu Dar es Salaam
Rais Jakaya Kikwete, Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana Sefue, wakipiga picha ya pamoja na Makatibu wakuu, baada ya hafla hiyo ya kumuapisha Katibu Mkuu Kiongozi iliyofanyika leo Ikulu Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana Sefue (kushoto) akifurahia jambo na Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Phillemon Luhanjo, wakati wa hafla hiyo ya kuapishwa katibu Mkuu kiongozi Ikulu Dar es Salaam leo.
Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Phillemon Luhanjo, akihojiwa na waandishi wa habari, mara baada ya kumalizika kwa hafla hiyo ya kumuapisha Katibu Mkuu Kiongozi mpya, Balozi Ombeni Yohana Sefue Ikulu Dr es Salaam leo.
Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Subscribe to:
Posts (Atom)


















