Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, January 3, 2012

RAIS KIKWETE AOMBOLEZA VIFO VYA AZIZ SHEWEEN NA BALOZI ATHUMAN MHINA

Rais Jakaya Kikwete, akiweka sahihi kwenye kitabu cha maombolezo ya kifo cha Aziz Sheween, Mikocheni jijini Dar es salaam, Jumatatu jioni nyumbani kwa marehemu Ofisa huyo wa Mambo ya Nje Mkuu Daraja la kwanza katika Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, aliyefariki dunia huko Riyadh, Saudi Arabia.
Rais Kikwete akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezo alipofika Madale jijini Dar es salaam, jana Jumatatu jioni nyumbani kwa Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Balozi Athumani Mhina aliyefariki dunia usiku wa kuamkia jana alipokuwa akipelekwa katika Hospitali ya Jeshi Lugalo kutibiwa shinikizo la damu.
Rais Kikwete, akiagana na baadhi ya wanafamilia ya marehemu ya Aziz Sheween, baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu huyo Ofisa Mambo ya Nje Mkuu Daraja la I katika Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, aliyefairiki juzi huko Riyadh, Saudi Arabia.
Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuia ya Wazazi ya CCM,
Balozi Athumani Mhina enzi za uhai wake.


KATIBU Mkuu wa Jumuia hiyo, Khamis Dadi alisema Balozi Mhina alifariki usiku wa kuamkia jana aliokuwa akipelekwa katika Hospitali ya Jeshi Lugalo kutibiwa shinikizo la damu.

Dadi alisema Mhina alikuwa akipelekwa hospitali baada ya hali yake kubadilika ghafla kutokana na maradhi ya shinikizo la damu.Alisema mwili wa marehemu, ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM, umehifadhiwa katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo na kwamba mazishi yake yanatarajiwa kufanyika kesho.


Dadi alisema marehemu atazikwa kijijini kwao Mnyuzi wilaya ya Korogwe mkoani Tanga na kwamba mwili wake utasafirishwa leo kwenda kijijini huko.Alisema kabla ya kusafirishwa, wakazi wa Dar es Salaam watapata fursa ya kutoa heshima za mwisho nyumbani kwake Mada

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...