Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, January 30, 2012

SUPER NYAMWELA ATAMBULISHA NYIMBO YAKE MPYA.

KIONGOZI wa wacheza shoo wa Bendi ya Extra Bongo,Hassan Mussa(Super Nyamwela) ametambulisha nyimbo yake mpya ya Bakutuka katika Ukumbi wa Mzalendo Pub Kijitonyama Jijini Dar es Salaam.
Akiimba sambamba na waimbaji wengine wakiwemo,Athanas Motanabe, Suleiman Ramadhan(Suzuki), Rama Pentagon,Frank Almas(Kabatano),Redo Mopasa (Mauzo), na Emanuel Michael (Bob Kissa) ambapo walimba sambamba na shoo kali ambayo iliwafanya mashabiki waliohudhulia onyesho hilo kuachia viti na kusimama.
Akizungumza na mtandao huu, Super Nyamwela amesema ameamua kuimba ili kuwapa mashabiki wake kachumbali na kuwazihilishi kuwa si kucheza tu bali hata kuimba pia anaweza.
Wimbo wa Nyamwela ndio unaofunga albam mpya ya Extra Bongo ambayo kwa sasa wako Studio wakiandaa Video yake ambapo tayari nyimbo mblili zimeshakamilika na tayari zimeashaanza kupigwa kwenye vituo vya Televisheni lakini bado hawajaipatia jina albam hiyo.
Nyamwela ambaye amedhamilia kuleta mapinduzi ya mziki wa dansi nchini na Dunia nzima kupitia Bendi ya Extra Bongo kwa sasa anaandaa shoo kali ya aina yake ambayo anasema itakuwa historia kwa watanzania na Dunia nzima.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...