Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, January 5, 2012

Majina ya walioteuliwa kushiriki kozi ya ngumi yatajwa


Na Mwandishi Wetu

SHIRIKISHO la Ngumi za ridhaa nchini (BFT) limepiga panga majina
matano kati ya 30 ya makocha walioteuliwa kushiriki katika kozi ya
kimataifa ya mchezo huo iliyopangwa kufannyika Januari 16 mwaka huu.
BFT imewakata washiriki hao baada ya Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC)
kuwataka BFT kupunguza idadi ya washiriki kutokana na hasara
iliyosababishwa na washiriki hao katika kozi ya awali iliyokuwa
ifanyike tangu mwezi Novemba mwaka jana.
TOC ambayo huandaa kozi za michezo mbalimbali kutokana na ruzuku
inayotolewa na Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa (IOC) ilikuwa iendeshe
kozi hiyo tangu mwaka jana lakini haikufanyika kutokana na mkufunzi wa
kozi hiyo kutoka nchini Algeria kuingia mitini.
TOC ililazimika kuwalipa nauli baadhi ya washiriki waliotoka nje ya
Dar es Salaa kutoka katika fungu la pesa za kuendeshea kozi hiyo
hivyo kuwataka BFT kupunguza idadi ya washiriki hasa wale waliofanya
utovu wa nidhamu katika kozi ya awali ili kiwango cha pesa kilichobaki
kutosheleza mahitaji wa kozi itakayoendeshwa Januari 16 mwaka huu.
Akizungumza Dar es Salaam Katibu mkuu wa BFT, Makore Mashaga alisema
idadi ya makocha 25 waliowateua inaweza ikapungua tena kulingana na
bajeti waliobaki nayo TOC ambapo hata hivyo hakuyataja majina matano
ya washiriki walioachwa .
Aliwataja washiriki waliopenya kuhudhuria kozi hiyo ni mpiga picha wa
Magazeti ya Busines Time, Majira, Sports Starehe na Jarida la Maisha
ambaye pia alikuwa bondia, Rajabu Mhamila 'Super D', Anord Ngumbi,
Moses Lema, Anthon Mwang'onda na Edward Emanuel (Dar es Salaam).
Wengine ni Yahaya Mvuvi (Tabora), Joseph Mayanga na Zakaria Mwaseba
(Morogoro), Omari Saady na Mussa Bakari (Mwanza), Ally Ndee (JKT
Mbeya), Emilio Moyo na Gaudens Uyaga (Pwani) Juma Liso (Magereza
Kigoma), Lyinda Kalinga (Dodoma) na Abdalah Bakari (Tanga).
Wengine ni Mohamed Hashim (Polisi Dar es Salaam), David Yombayombam,
Haji Abdalah, Said Omari (JWTZ), Mazimbo Ally, Rogated Damian na
Fatuma Milanzi (JKT), Musa Maisori na Hamisi Shaaban (Magereza Dar es
Salaam).
Kozi hiyo itaendeshwa na mkufunzi wa kimataifa Josef Diouf kutoka
Shirikisho la Dunia la mchezo huo (AIBA) ambaye atashirikiana na
makamu wa Rais wa BFT, Michael Changarawe.
Kozi hiyo itafanyika latika shule ya Sekondari ya Filbert Bayi Kibaha
Mkoani Pwani na itafikia tamati Januari 24 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...