Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, January 30, 2012

MISS KISWAHILI ASHEREHEKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA NA WATOTO YATIMA


MISS Kiswahili Tanzania, Rehema Fabian amesherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa aina ya pekee ambapo amejumuika na Watoto Yatima wa Kituo cha Kuwama kilichopo Mwenge Jijini Dar es Salaam
Akizungumza na mtandao huu Rehema amesema nimefanya hivi ili kuikumbusha jamii haswa Warembo wenzangu na Mastaa kwa ujumla kuwa kuna wenzetu ambao wanahitaji faraja ya pekee na haswa tunapowashirikisha furaha zetu kama hivi
Watu wengi wanapokuwa na furaha binafsi hujumuika na ndugu ama marafiki na kufanya makamuzi ya kufa Mtu lakini pia tunapowakumbuka hawa ambao hawamjui Mama wala Baba ni jambo jema mbele ya jamii na kwa Mwenyezi Mungu pia
Rehema Fabiani ni Mrembo anayeshikilia taji la Miss Kiswahili Tanzania kwa sasa,wito wake kwa jamii ya watanzania na haswa kwa watu wenye uwezo ama nafasi tuwakumbuke watoto Yatima amesema Rehema

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...