Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, January 12, 2012

USAFIRI WA RELI YA KATI KUANZA HIVI KARIBUNI
Naibu Waziri wa Uchukuzi Athumani Mfutakamba amesema usafiri wa reli ya kati uliokuwa umesitshwa kwa muda unatarajiwa kurejea tena baada ya kazi ya matengenezo ya maeneo yaliyoharibiwa na mvua katika stesheni ya Gulwe na Godegode kukamilika kwa asilimia 80.


Dk Mfutakamba alieleza hayo wakati akizungumza na uongozi wa reli ya TRL karakana ya Morogoro mara baada ya kutembelea karakana hiyo kuona shughuli mbalimbali za utengenezaji na ufufuaji wa injini za treni ukiendelea.

Dk. Athumani Mfutakamba alifanya ziara hiyo baada ya Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) kufanya zoezi la kuwarejeshea nauli zao wasafiri wapatao 1920 ambao walikuwa wasafiri na treni kutoka Dar kwenda Kigoma siku za Jumamosi Jan 07, 2012 na Jumanne Jan 10, 2012 ambazo zimelazimika kufutwa baada ya reli ya kati kuharibika.
Ambapo pamoja na mambo mengine alisisistiza umuhimu wa wahandisi wa karakana hiyo ya TRL kuharakisha ufufuaji wa injini kutokana na uhitaji mkubwa uliopo wa ubebaji wa mizigo na abiria kwa gharama nafuu katika reli hiyo ya kati kwa wakazi wa mikoa ya Tabora na Mwanza.

Pia aliwataka wataalamu hao wa TRL kutumia vipuri vya ndani ya nchi kwa kushirikiana na shirika la mzinga na mang'ulaili kupunguza gharama badala ya kuagiza kutoka nje.

Kwa upande wake meneja wa karakana ya TRL Morogoro mhandisi Ngosa Ngosomwile alisema kuwa tayari serikali imeipatia kiasi cha shilingi bilioni 4.2 kwa kupitia kampuni ya kusimamia mali za shirika la reli RAHCO kwaajili ya matengenezo ya injini 5 na kununua vipuri vya magari yanayoendelea na kazi.

Aidha ameomba vipuri vinavyoshikiliwa na RAHCO wapatiwe ili viweze kutumika katika kukarabati baadhi ya injini.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...