Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, January 11, 2012

MBUNGE VICK KAMATA AKABIDHI BAISKELI 30 KWA WALEMAVU GEITA
Mwenyekiti wa Victoria Foundation Mh. Bi. Vick Kamata yuko Geita kwa wananchi wake kama anavyoonekana pichani akikabidhi baiskeli kwa walemavu 30 wa tarafa ya Bugando wilaya ya Geita mkoa mpya wa Geita. Hizi ni moja ya juhudi za mbunge huyo kwa wananchi wake katika kusaidia kuondoa matatizo yanayowakabili watu wenye ulemavu wa viungo ambao wamekuwa wakikabiliwa na matatizo mengi ukiwemo usafiri kama hizi baiskeli zitakazowasaidia kwenda hapa na pale na kuendelea na shughuli zao. Hapa anaonekana akifurahia jambo na mmojwa wa walemavu waliokabidhiwa baiskeli hizo na mbunge huyo.

Mh. Vick Kamata akizungumza na mmoja wa wazee wa Geita.

Vick Kamata akimsaidia kusukuma baiskeli hiyo mmoja wa walemavu mara baada ya kumkabidhi baiskeli hiyo.

Baadhi ya walemavu wakiwa na baiskeli zao mara baada ya waliokabidhiwa.

Vick Kamata akifurahia jambo na mmoja wa walemavu hao.

Vick Kamata akizungumza na wananchi wakati alipkabidhi baiskeli za walemavu huko Geita.

Baadhi ya walemavu wakisubiri kukabidhiwa baiskeli na mbunge Vick Kamata.

Baadhi ya baiskeli zilizokabidhiwa kwa walemavu huko Geita,

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...